BWANKU M BWANKU
JF-Expert Member
- Jan 12, 2019
- 377
- 435
Leo Jumatano Machi 23, 2022, Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kuzindua Nyumba 644 za Makazi Magomeni Kota Jijini Dar es Salaam kuanzia Saa 4 na nusu asubuhi hii.
Utafuatilia Matangazo haya ya moja kwa moja kupitia Televisheni, Radio na Mitandao ya Kijamii.
#TunaImaninaSamia
#Siku365zaRaisSamia
#KaziInaendelea.
UPDATES
Alichoongea Rais Samia
Mradi huanza na wazo wazo hili la utekelezaji wa ilani ya uchaguzi kama ilivyagizwa kwenye kile kifungu cha 55H kifungu kidogo cha pili, Wazo hili lilianza kutaka kutekeezwa na mtangulizi wangu Hayati John Pombe Magufuli na yeye ndiye aliyeanzisha mradi huu. Angependa leo awepo hapa kuuzindua mradi huu na kutimiza ahadi alizoziweka kwa Wananchi wa Magomeni lakini Mungu ana maamuzi yake nasi tumeyapokea.
Ndugu Wananchi baada ya kupata mualiko kutoka kwako Waziri nimeona ni vyema nikaungana nanyi katika jambo hili na ukubwa wake katika historia ya nchi yetu lakini pia historia ya Wananchi wanaoishi eneo hili.
Serikali inatambua umuhimu wa makazi bora kwa waazi wake ambapo mahitaji ya nyumba bora yanakadiriwa kuwa zaidi ya milioni 3, Kila mwaka tunakisia kuwa na mahitaji ya nyumba laki 2. Sasa kasi yetu ya ujenzi na kasi ya mahitaji ya nyumba hayaendani. wahiyo tuna kila sababu ya kufanya bidii na kutekeleza lililoagizwa na ilani ya uchaguzi kwamba tuongeze kasi katika kujenga makazi tena makazi bora kama haya hapa kwa ajili ya wananchi wetu.
Niseme nimefurahishwa sana na usanifu na ujenzi wa maghorofa uliofanywa na Wakala wa majengo TBA wakisaidiana na mawakala wengine wafanyakazi mbalimbali hapa chini ya usimamizi wa Wizara ya Ujenzi na uchukuzi. Nimefurahishwa zaidi na ubunifu na hekima iliyotumika kupambana na changamoto mbalimbali lakini ujenzi huu ukamilike.
Hatua hii ya ujenzi wa maghorofa katika mradi huu ni matokeo ya utekelezaji wa sera ya matumizi bora ya ardhi ili wananchi wengi waweze kunufaika na miradi ya namna hii. Baada ya chokochoko alizozisema Mkuu wa Mkoa lakini kulikuwa na maneno mengi kwamba miradi haitoendelea. Ukiuliza kwanini kulikuwa hakuna sababu.
Miradi hii imeandikwa na kuagizwa katika ilani ya CCM, serikali zote zinazoongoza Tanzania ni za CCM, awamu moja ikiondoka awamu ya pili inashika serikali ya CCM. Kwahiyo wanaposema miradi haitakamilika, upeo wao ni mdogo sana na kwamba hata miradi hii ilianzishwa awamu ya tano mimi nilipokuwa Makamu wa Rais, kwahiyo ni sehemu ya miradi hiyo kuanza kwake na kutekelezwa kwake.
Ndugu Wananchi Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi katika taarifa yake ameeleza historia nzuri sana katika uanzishaji na uendelezaji wa maeneo haya ya kota mbalimbali kwa ajili ya wafanyakazi, serikali ya ukoloni ilikuwa na mpango wake na sasa serikali yetu ina mpango wake.
Kabla ya kuja hapa nimepata muda wa kuzungukia katika nyumba hizi, ni nyumba nzuri, zimejengwa kisasa nyumba ambazo zitakidi mahitaji ya watakao kaa hapa. Langu kwenu ni utunzaji wa nyumba hizi, maana tumefanya mnachohitaji. Kwa sababu nyumba hizi wanakaa watu wengi usafi hasa maeneo ya kodido na ngazi unaweza kuwa changamoto.
Mh. Waziri nimepata maombi pia kutoka TBA ya kutoa pesa zaidi kwa ajili ya kujenga katika maeneo yaliyowazi yaliyotolewa na Tamisemi. Hii nataka nisema kwamba Sekta Binafsi popote wanapoona wanaweza kuweka fedha wafanye hivyo, hivi navyozungumza Sekta Binafsi wapo tayari kushirikiana nanyi TBA na kujenga maeneo yote ambayo mtasema yanahitaji kujengwa. La maana hapa ni kukaa vyema kujadliana na kukubaliana kwa mikataba yenye tija.
Niwapongeze TBA kwa kupata wazo la kuweka Machinga Complex hapa hapa, pia niwapongeze kwa kuweka Super Market hapo lakini nitoe wazo la kuweka parking hapa hapa ziwe parking za kisas zitakazoweza kuweka gari nyingi na sio zile za kuweka mistari tu na hii itakuwa kitega uchumi chenu TBA.
Wananchi mliniomba kupewa nyumba hizi kwa utaratibu wa Mpangaji mnunuzi, sasa niseme kwamba nimeridhia ombi lenu la kupewa nyumba hizi kwa utaratibu wa mpangaji mnunuzi na kurejesha gharama za nyumba pekee hatutawatoza gharama za ardhi kwa sababu tukifanya hivyo mtashindwa kuzinunua.
Jengine kwa wale wanaotaka kuweka pesa zao polepole waanze kulipa sasa polepole, itakapofika miaka mitano kama haijakamika utaendelea kulipa polepole.
Baada ya kusema haya, nyumba tayari nimeshazifungua niwatakie kila la kheri wale ambao wataingia kwenye nyumba hizi, niwaombe mkaishi kama ndugu. Watoto watakaokuwa hapo walelewe na wote.