Rais Samia: Barabara ya Tabora - Mpanda Unateleza na lami tu

Rais Samia: Barabara ya Tabora - Mpanda Unateleza na lami tu

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan ameeleza kuwa Serikali inaendelea kuboresha miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Katavi ambapo sasa barabara ya kutoka Tabora hadi Mpanda (km 352) ni ya kiwango cha lami.​

Rais Dkt. Samia ameeleza hayo leo Julai 13, 2024 wakati akizungumza na wananchi wa Inyonga Wilayani Mlele wakati wa ziara yake mkoani Katavi.

“Wakati nimekuja kipindi cha kampeni kutoka Tabora kwenda Mpanda ilikuwa ni vumbi tupu lakini leo nimeteleza mpaka nimesinzia, Barabara ni nzuri na ni maendeleo makubwa sana, Niwapongeze sana”, amesema Dkt. Samia.

Dkt. Samia ameeleza miradi mingine inayoendelea kutekelezwa na Serikali katika Mkoa wa Katavi ni pamoja na ujenzi wa barabara ya Kibaoni - Makutano ya Mlele (km 50), Vikonge - Luhafwe (km 25), Luhafwe - Mishamo (km 37) na Kagwira - Karema (km 110) kwa kiwango cha lami.

Aidha, Dkt. Samia ameeleza kuwa pamoja na miradi inayoendelea kutekelezwa, Serikali ipo katika hatua za kutafuta Makandarasi wa kutekeleza miradi mingine ya miundombinu ya barabara katika Mkoa wa Katavi.

Ametoa wito kwa Wananchi wa Mkoa wa Katavi kutunza na kulinda miundombunu ya Barabara iliyokamilika na inayoendelea kutekelezwa.
 

Attachments

  • RAIS SAMIA - BARABARA YA TABORA - MPANDA UNATELEZA NA LAMI.MP4
    27.6 MB
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.24.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.24.jpeg
    263.2 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.25.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.25.jpeg
    315.9 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.25(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.25(1).jpeg
    722.1 KB · Views: 8
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.26.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.26.jpeg
    922.4 KB · Views: 6
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.26(1).jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.26(1).jpeg
    805 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.26(2).jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.26(2).jpeg
    579.5 KB · Views: 4
  • WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.27.jpeg
    WhatsApp Image 2024-07-13 at 15.32.27.jpeg
    423.8 KB · Views: 4
Kasheshe barabara ya mpanda hadi uvinza la kuna eneo hilo ni balaa huamini kabisa kuwa kweli ni Tanzania hii hii au wale ni raia wa nchi zingine barabara ilivyo mbovu
 
Back
Top Bottom