Ngosha Mashine
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 665
- 1,360
Kitu pekee Mwl Nyerere alikosea na nadhani anajutia hata huko aliko ni kuipa nguvu sana CCM
Chama kimekuwa na nguvu sana kuiongoza serikali, na ni Chama hiki hiki chenye wanachama wengi wafanyabiashara na wawekezaji wengine wa kawaida kuliko wasomi (wabebovu wa masuala fulani kielimu).
Chukulia mfano kanda ya ziwa tu ina wabunge karibia sita wa darasa la saba (Msukuma, Kishimba, Tabasamu kuna yule wa Nyangh'wale n.k) eti hawa ndio waje kuiongoza serikali kisa wamebahatika tu kuwa na rasilimali fedha.
Sasa hivi nchi yote kuanzia serikali za mitaa na kata, wenyeviti na madiwani 99% nchi nzima ni CCM sasa hebu zunguka ukaone elimu zao 70% yao ni la saba na ndio hawa hawa ambao wanaidharau elimu yetu ambayo chama chao ndio kinaitoa nchini kwetu, chukulia mfano mbuge Msukuma anavyowabeza wasomi hivi unadhani huyu la saba anaweza kweli kupokea michango ya kimawazo ya waliosoma (wasomi) jimboni kwake?
Hawa la saba ndio wanaongoza mabaraza ya mitaa, kata, halmashauri zetu na hata bunge lenyewe bahati mbaya wanaguvu ya kichama tawala yaani huwafanyi kitu wakiamua jambo.
Sasa hivi kuna hili la wanaodai katiba najua Rais Samia haikuwa nia yake kupinga ila nguvu ya chama chake imemmeza na yeye kakubali kutekeleza mapendekezo ya chama chake.
Nadhani hapa sijaeleweka ipo hivi katiba ilikuwa kidogo ipite kwa Rais mstaafu Jakaya ila hapo ndio chama kilitumia nguvu kubwa kumpinga Rais na maamuzi yake ya kuruhusu mchakato wa katiba ikaibuka migogoro na hapa na pale mchakato ukapotea.
Ushauri wangu kwa Rais Samia hii nguvu ya chama chako kukulazimisha uendeleze ubabe, utawafunga sana wapinzani n.k lakini upinzani hautaisha kwame na hii itakuharibia wewe na sio hao wanaokusukuma kufanya hayo maana watu hawawajui hao zaidi wanakujua wewe maana ndio kiongozi wa juu, Mh Rais wewe angalia nini ni cha mhimu kwako na ni kipi watu wanataka usiwasikilize sana hao wanaokusukuma kufanya ubabe ili kulinda masirahi yao binafsi.
Utaondoka utawaacha na hawatakukumbuka kwa lolote, najua wanakutisha na wewe mh Rais unaogopa kupoteza uongozi 2025 lakini wewe fanya kile kinachompendeza Allah wewe ni mtu wa dini!
Nasikitika kuona hata haujali, labda nikuambie mh Rais, Hayati Rais Magufuli asinge kufa ni lazima angeleta mchakato wa katiba kati ya 2023-2025 hii angeifanya ama kujiongezea mda wa kukaa madarakani au kama anaondoka kumfunga Rais ajaye asiharibu kile alichokianzisha.
Maana **** ni reli ilikuwepo, kama ni ndege zilikuwepo ila hapa katikati zilikufa sasa yeye (JPM) asingekubali kuona vitu alivyovipigania vinakufa hivyo mchakato wa katiba ulikuwepo pale pale.
Huku mtaani watu wa chama chako walikupinga toka mwanzo baada ya kuona kama unataka usawa najua unajua chama chako hakitaki usawa, ili CCM iendelee kuwepo haitaki usawa kabisa na ndio maana ili kulinda masirahi yao hawakukuunga mkono walianza kupandikiza chuki dhidi yako kwa wananchi.
Pamoja na kwamba umeanza kufuata nini wanataka chama chako, ila bado chuki ipo miongini mwa wananchi walio wengi mh hili la chanjo raia hawakuelewi kabisa waliaminishwa chanjo zina madhara hivyo wameanza kuona wewe kama kibaraka.
Kama umeamua kukifuata chama chako hebu kuwa kama mtangulizi wako machinga wawe huru, tumbua (kariakoo kwa huo moto angekuwa JPM kuna watu wangekuwa mtaani mpaka mda huu ila wewe upo kimya) lakini wewe umeona kuwafunga kina Mbowe na kuzuia katiba tu ndio itakusaidia la ha shaaa!
Kuwa sehemu moja ueleweke kama unafuata ya mtangulizi wako ama umeamua kuwa na usawa
Uwe na Kazi njema mh Rais