Rais Samia: Hakuna ulazima wa Magari kukaguliwa hapa nchini

Dr Restart

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2021
Posts
4,949
Reaction score
24,046
Leo baada ya CAG Kichere kuwasilisha ripoti ya ukaguzi wa hesabu za serikali, Mh Rais alipata nafasi ya kutia neno.

Mh Rais ameona hakuna ulazima wa magari kukaguliwa hapa nchini. Ameona umuhimu ni magari kukaguliwa huko huko yanapoagizwa.

Mh Rais amesema wenzetu wapo makini kwenye kufanya ukaguzi. Wanafanya kwa kufuata taratibu stahiki na hawapo tayari kuharibu biashara yao.

Hivyo, ameshuri kuwepo na agency ya kufanya ukaguzi huko nje. Ili gari likifika hapa nchini ifike na Certificate ya ukaguzi na iruhusiwe kuingia nchini.

Ameongeza kuwa, ukaguzi hapa nchini unaleta urasimu usio na lazima na kuongeza mianya ya rushwa.

Kiukweli jambo hili ni la kupigiwa makofi. Kulikuwa na upuuzi usio na mantiki kwenye ukaguzi wa magari hapa nchini.

Kongole Mh Rais
 
Idea ilikua ile pesa ya ukaguzi na ajira zibaki hapa hapa inchi...that's how you add value to your economy.

Hivi huyu mdudu aliezilemaza akili zetu kua watu wa inje wanafanya kazi nzuri kuliko ss ni nani?kwann tusizifanyie kazi changamoto zetu tukawa efficient?

Tukiendelea hivi nadhani ni vyema na haki serikali nayo tuka i out source nje ya inchi maana huko kuna walio waaminifu, wabunifu na efficient kuliko sisi.
 
Umemuangalia mnunuaji? gari ije mbovu hapa alafu ikataliwe au imgharimu pesa nyingi kwenye matengezo.. ila kama inafanyiwa kule huo msala hauwezi muangukia
 
Idea ilikua ile pesa ya ukaguzi na ajira zibaki hapa hapa inchi...that's how you add value to your economy. Hivi huyu mdudu aliezilemaza akili zetu kua watu wa inje wanafanya kazi nzuri kuliko ss ni nani?kwann tusizifanyie kazi changamoto zetu tukawa efficient...
Tujenge kwanza image nzuri kuwa kweli hapa tuna uwezo wa kuifanya hii kazi kwa unanimity bila rushwa, hapa ni rushwa tupu...na ningependa hii kazi ya kukagua magari iondolewe traffic department na wapewe watu binafsi wenye utaalam huu,welldone my president hapa umenena, pls next iwe TRA na cousins wao TBS kumeoza mno
 
Idea ilikua ile pesa ya ukaguzi na ajira zibaki hapa hapa inchi...that's how you add value to your economy.
Hivi huyu mdudu aliezilemaza akili zetu kua watu wa inje wanafanya kazi nzuri kuliko ss ni nani?kwann tusizifanyie kazi changamoto zetu tukawa efficient?
Tukiendelea hivi nadhani ni vyema na haki serikali nayo tuka i out source nje ya inchi maana huko kuna walio waaminifu, wabunifu na efficient kuliko sisi.
Unafanyaje ukaguzi baada ya gari kufika?

Tangu lini ukalikagua gari baada ya kununua?

Kama unataka kuongeza value kwenye uchumi, kampuni za nchi yetu ziende huko. Ziombe leseni ya kufanya ukaguzi za magari yatakayoagizwa na Watanzania.
 
Kama unataka kuongeza value kwenye uchumi, kampuni za nchini yetu ziende huko. Ziombe leseni ya kufanya ukaguzi za magari yatakayoagizwa na Watanzania.
This is good argument...kampuni za kitanzania ziende nje kuliko habari ya kuwapa wajapani hio kazi then tunazunguka mlango wa Nyuma kutembeza bakuli...

Bt again nani alishawahi kununua gari mtandaoni lika fail inspection zao huko?
By the time unanunua gari mtandaoni hao wa mitandaoni washalinunua kwenye mnada at a cheap price na likafanyiwa ukaguzi then wakaliweka kwenye website, ukaguzi tunaofanya sisi ni km fomality..
 
Tujenge kwanza image nzuri kuwa kweli hapa tuna uwezo wa kuifanya hii kazi kwa unanimity bila rushwa, hapa ni rushwa tupu...na ningependa hii kazi ya kukagua magari iondolewe traffic department na wapewe watu binafsi wenye utaalam huu,welldone my president hapa umenena, pls next iwe TRA na cousins wao TBS kumeoza mno
Hizi ndo changamoto zenyewe za kufanyiwa kazi...you dont give it up, work on it...imagine jamaa alievumbua bulb akaacha project yake just after a 3rd test.

Nothing is impossible labda kufufua mtu.. km Rwanda Rushwa ni km haipo sisi tunashindwa nn?
 
  • Thanks
Reactions: Tsh
Ni sahihi

Siku zote bidhaa inakaguliwa pale pale ilipouzwa na kama haifai unaachana nayo

Umeagiza gari inafika Dsm ndo unaambiwa haina hiki na hiki ili iweje na ushaingia gharama?

Halafu kubwa zaid ni Rushwa rushwa tu…gari unaambiwa haiwezi kutoka tyre hazifai kanunue mpya…kumbe magumashi wanataka Rushwa, ukiwapa Laki wanaruhusu Gari itoke na hizo hizo tyre
 
Idea ilikua ile pesa ya ukaguzi na ajira zibaki hapa hapa inchi...that's how you add value to your economy.
Hivi huyu mdudu aliezilemaza akili zetu kua watu wa inje wanafanya kazi nzuri kuliko ss ni nani?kwann tusizifanyie kazi changamoto zetu tukawa efficient?
Tukiendelea hivi nadhani ni vyema na haki serikali nayo tuka i out source nje ya inchi maana huko kuna walio waaminifu, wabunifu na efficient kuliko sisi.
Gari likija likawa bovu linarudi au linarekebishwa? Anayelipia hayo marekebisho ni mnunuzi au muuzaji? Tukiwa na haya majibu turudi kuangalia kama alichofanya ni upuuzi au ni kweli ni kutengeneza mazingira ya rushwa tu.
 
Hizi ndo changamoto zenyewe za kufanyiwa kazi...you dont give it up, work on it...imagine jamaa alievumbua bulb akaacha project yake just after a 3rd test...
Nothing is impossible labda kufufua mtu.. km Rwanda Rushwa ni km haipo sisi tunashindwa nn?
Nakubaliana nawe ila inabidi tuanze upya na tuipige hii cancer inayoitwa rushwa, tuanzie kwenye family zetu na mashuleni, Botswana 🇧🇼 wapo super 👌, rushwa it's almost zero
 
Unafanyaje ukaguzi baada ya gari kufika?

Tangu lini ukalikagua gari baada ya kununua?

Kama unataka kuongeza value kwenye uchumi, kampuni za nchi yetu ziende huko. Ziombe leseni ya kufanya ukaguzi za magari yatakayoagizwa na Watanzania.
nilikuwa nashangaa kitu hiki
vp gari ikakutwa na hitirafu na ishaingia nchini itarudishwa huko ?
 
Ilikuwa ikikutwa na hitilafu uaambiwa 'jiongeze' na balaa zaid unakuta agent wako wa kutoa gari ndio anashirikiana na wakaguzi kukutoa pesa za Rushwa

Wakati nwingine kila kitu kipo sawa lakin wanakuchekecha utoe pesa tu

Wakaguzi wakakae huko huko na ukaguzi ufanyike bila ya kuonana na mnunuzi kupunguza mianya ya Rushwa
nilikuwa nashangaa kitu hiki
vp gari ikakutwa na hitirafu na ishaingia nchini itarudishwa huko ?
 
Idea ilikua ile pesa ya ukaguzi na ajira zibaki hapa hapa inchi...that's how you add value to your economy.

Hivi huyu mdudu aliezilemaza akili zetu kua watu wa inje wanafanya kazi nzuri kuliko ss ni nani?kwann tusizifanyie kazi changamoto zetu tukawa efficient?

Tukiendelea hivi nadhani ni vyema na haki serikali nayo tuka i out source nje ya inchi maana huko kuna walio waaminifu, wabunifu na efficient kuliko sisi.
nimekuelewa kiongozi, lengo la kupima magari baada ya kufika hapa nchini ilikuwa ni mkakati wa JPM kutoa ajira kwa watanzania pia kuhakikisha kuwa magari yote yanayoingia hapa nchini ni bora kulingana na viwango tulivyojiwekea. Mawakala wa nje kiukweli hawapimi, kilichochokuwa kinafanyika ni kutoa fedha na kupewa cheti cha kufaulu. Waagizaji wa jumla wa magari watalisemea hili. Kilichopo ni madalali wa mawakala hawa wamepata upenyo wa kumshauri raisi ili waendelee na 10% walizokuwa wamezimiss. POOR TANZANIA!
 
Umemuangalia mnunuaji? gari ije mbovu hapa alafu ikataliwe au imgharimu pesa nyingi kwenye matengezo.. ila kama inafanyiwa kule huo msala hauwezi muangukia
Hata hayo makampuni yanayouza magari kama beforward waweke certificate of inspection kwa kila gari wakiwa wanaiweka kwenye website yao.
 
Nayo ni nzuri.. ila gari lazima uone ni grade gani unapotaka kununua.. maana kuna 5.0, 4.5 na kuna 4.0 na zipo kushuka hapo unajipimia mwenyewe
 
nimekuelewa kiongozi, lengo la kupima magari baada ya kufika hapa nchini ilikuwa ni mkakati wa JPM kutoa ajira kwa watanzania pia kuhakikisha kuwa magari yote yanayoingia hapa nchini ni bora kulingana na viwango tulivyojiwekea. Mawakala wa nje kiukweli hawapimi, kilichochokuwa kinafanyika ni kutoa fedha na kupewa cheti cha kufaulu. Waagizaji wa jumla wa magari watalisemea hili. Kilichopo ni madalali wa mawakala hawa wamepata upenyo wa kumshauri raisi ili waendelee na 10% walizokuwa wamezimiss. POOR TANZANIA!
Ajira zenyewe zipo ngapi?

Huo ukaguzi ni kwa gharama ya usumbufu na rushwa? Unaajiri watu wakulazimishe utoe rushwa?

Bora hizo ajira zisiwepo kwa lengo la kupunguza rushwa na usumbufu bandarini.
 
Back
Top Bottom