Mama Samia rais wetu, umetufahamisha rasmi uwepo wa ugonjwa huu mbaya hapa nchini. Umetaka maelekezo yote yanayotolewa na wataalamu kufuatwa. Kwa mioyo mikunjufu yote tumeyakubali na tutayazingatia.
Tunaamini maelekezo yako ndiyo ulio msimamo rasmi wa Serikali na kuwa hayatakuwa maneno matupu yasiyoweza kuvunja mfupa.
Si nia yangu kuyarejelea yote wanayotutaka wataalamu kuyazingatia. Bali yale ambayo yanahitaji msukumo wako wewe kama kiongozi wetu.
Ndani ya wiki moja Hospitali ya Bugando imepoteza madaktari bingwa 2. Kwa hakika mpambano na ugonjwa huu si mwepesi hata kidogo. Msukumo wako zaidi unahitaji utakaosaidia kuyaweka mambo kuwa sawa zaidi ikiwamo kuokoa muda.
Tumefika je hapa tulipo? Hakuna mwenye akili zake asiyejua. Hofu ya watawala ilikuwa imetamalaki. Huu utakuwa ni muda wa kusukuma vilivyo hali ile kubadilika. Kwenye maeneo yao watu wahimizwe kutekeleza wajibu wao kikamilifu bila ya kukusubiria wewe kuingilia kati.
Katika maelekezo ya wataalamu kuhusiana na ugonjwa huu, inafahamika kuwa:
1. Takwimu za ugonjwa zinapaswa kutolewa na kwa wakati.
2. Misongamano isiyo ya lazima kusitishwa.
3. Social distancing na barakoa kutumika kote inapobidi.
Itifaki rasmi za kuyafanikisha haya zinapaswa kuwapo na kujulikana wazi wazi na kila mtu. Ambapo:
#1. Itaweka dira na msisitizo zaidi wa namna ya kujihami na kuwahami wengine, kwa maeneo kulingana na kiwango cha uathirika.
#2. Mikusanyiko yote isiyo ya lazima zikiwamo sherehe, misiba, ibada nk kufuata itifaki rasmi zinazofahamika.
#3. Hili na yote hapo juu hayawezi kuwa hiari tena. Hii ikiwa ni kwa mustakabala mwema tu wa maisha yetu sote.
Mama umethubutu na kwa kwa pamoja tutavuka.
Nisiache kukusalimu kwa jina la JMT.
Ninawasilisha.