Kichuchunge
JF-Expert Member
- Dec 2, 2020
- 384
- 970
Rais Samia, Labda pengine wengine wanakuogopa. Au tuseme wanashindwa kukufikishia ujumbe. Lakini mimi, kwa unyenyekevu kabisa, nimeona kupitia safu hii niwe nakupenyezea yale ambayo yanasemwa huku mtaani lakini wasaidizi wako hawakufikishii ipasavyo.
Mama, kabla sijatiririka mengi kwanza nianze na hili lililozuka hivi karibuni la vikundi vya watu fulani fulani kujiunda kisha wakasema kuwa eti wao ni chawa wa mama. Mama si mwingine eti ni wewe! Labda nikuulize kitu mama; ni kweli wewe ndiye uliyewatuma waunde hivi vikundi?
Wanaweza kuwa wameviunda kwa nia njema lakini mapokeo yake yakawa mabaya kwa jamii. Huku kwetu mtaani watu wakisikia chawa wanatafsiri kuwa hawa ni wapambe tu wanaojua kupiga domo ili waweze kula. Wanatumia 'DOMOKRASIA' kwa ajili ya kuridhisha 'TUMBOKRASIA.'
Chawa wanaweza kuwa wazuri kwa afya ya kisiasa, lakini wasiwe wazuri kwa afya ya kijamii. Kiafya, hebu tuanzie hapa kwanza. Chawa ni nini? Ni mdudu anayependa kukaa kwenye uchafu. Hakai kwa watu wasafi. Hutaga mayai mwilini na kwenye nywele. Hufyonza damu na kuwasha ngozi. Mtu akijikuna, upele hufuata. Huchangia kueneza magonjwa pia. Mtu msafi hakai na chawa!
Kibinadamu Chawa ni mtu anayejipendekeza kwa mtu mwenye pesa au umaarufu na kumsifia kinafiki ili mradi tu afaidike naye kwa kulipwa fedha au kununuliwa vitu vidogovidogo au naye awe maarufu.
Mama kaa utafakari. Pengine hawa chawa ni wale wa 'Kikulacho ki nguoni mwako.' Inawezekana tayari watu wameishaona kuna fursa fulani kujiita chawa. Usistaajabu ukisikia bilioni kadhaa zimetumika kuhudumia hao machawa katika shughuli fulani ya uzinduzi wa mradi fulani.
Watu wameamua kutambua ulimbukeni na kujikomba kinafiki kwa wenye navyo kuwa ni ajira rasmi inayotambulika na wakubwa. Mama usikubali. Watalitumia vibaya jina lako.
Pengine watu wako hawakwambii, lakini mimi nimeona nikwambie. Mama sidhani kama haya yanayoendelea kutokea nchini hauyaoni. Haya ya watu kukamatwa, kutekwa, kupigwa na wakati mwingine hadi kuuawa kikatili.
Yalianza taratibu siku za nyuma, lakini kadri siku zivavyozidi kwenda yanazidi kushamiri. Mwanzoni mama uliwahi kuyakemea huko nyuma wakati ukiongea na Machifu wa makabila balimbali kule Tabora, ukitaka wakusaidie ingawa ukasema kuwa matukio kama hayo, mengine huwa ni 'drama' tu za watu.
Lakini siku zilivyozidi kwenda, tumeshuhudia watu wakizidi kutekwa, kuuawa pia, na wengi wao wakiwa ni viongozi wa vyama vya upinzani hususan Chadema.
Alianza kutekwa kiongozi wa vijana wa Chadema wilaya ya Temeke, Deusdedith Soka pamoja na wenzake. Watu wakapiga kelele lakini kimya. Hawajulikani walipo hadi hii leo. Haijulikani wako hai au wamekufa. Majuzi tena aliyekuwa kada wa Chadema, Ali Mohammed Kibao akatekwa na kuuawa kisha akatupwa.
Kibao, aliyekuwa Mjumbe wa Sekretarieti ya Chadema alichukuliwa jioni ya Septemba 6, 2024 eneo ya Kibo Complex Tegeta jijini Dar es Salaam na watu wasiojulikana, akiwa safarini kutoka Dar Salaam kuelekea Tanga na basi la Tashriff na mwili wake kupatikana Jumapili Septemba 8, 2024 eneo la Ununio, Dar es Salaam kisha kuzikwa Tanga Jumatatu.
Safari hii tena mama ulitoa pole na kukemea vitendo kama hivyo kwa kuagiza vyombo vya uchunguzi kukuletea taarifa ya kina kuhusu tukio hili baya kabisa na mengine ya namna hii haraka. Ukadai nchi yetu ni ya kidemokrasia na kila raia ana haki ya kuishi. Kwamba serikali unayoiongoza haivumilii vitendo vya kikatili vya namna hii. Kauli thabiti kabisa.
Ila mama fanya kitu. Toa uchafu na safisha kabisa jeshi la polisi, Wizara yake na ikibidi taasisi zote za usalama. Ni kosa kubwa sana kuruhusu taasisi zikaaongozwa na watu wasiojali. Asiyejali anawaagiza wasiojali wenzake kuvuruga amani. Wanakuja kwa staili ya chawa kama vile wanakusaidia wewe mama, lakini kumbe wanakuharibia. Reasoning yao kichwani ni zero! Sasa kufanya wanachokifanya inaweza ikawa ndiyo chanzo cha kuvuruga amani tuliyonayo.
Watu wakijaribu hata siku moja wakaingia barabarani wajue ikulu hapatakalika. Waache kuishi kwa mazoea.
Watanzania wamevumilia mengi sana. Wako kimya. Wengine hawana kazi za kufanya na hawana tumaini la maisha.
Kwa hiyo hawataona tabu kumla mamba majini huko huko wala hatafika nchi kavu.