Rais Samia hawa watu usipowateua watageuka kuwa maadui zako


Upumbavu tu huu! Mbona walimgeuka jiwe na mwisho wa siku kashinda kila kitu Mpaka uwakilishi mbinguni na sasa yuko huko anaendelea kutumbua
 
Adui wa Rais?

Ebu watume cv zao wapewe kazi kama waomba kazi tu. Wakikosa waungane na waliokosa tu.
 
Kufanya uandui ndani ya CCM ni kazi bure, kwa madaraka aliyonayo Mwenyekiti wetu ni sawa na kujisumbua tu, so wananchama wenzangu wa CCM cha kufanya ni kutii bila shuruti huku ukisubiri nafasi yako ya uteuzi kama itakuja ama lah, kama hili hutaliweza basi the only option ni kubakia kimya. Uamuzi ni wako.

Pelekeni ujumbe huu kwa wale vidomodomo, dawa yao tunaipika.
 
Yaani umewataja na watu ambao waliunga JUHUDI?Hawa kina MwEmbe walinunuliwa na walishalipwa chao,hawana deni kwa mama,kina KITAMBI wote hatakama walipewa nafasi ila walikula chao hawa "mercenaries"
 
Acha upopoma
 
Tuache ujinga wa kugawa vyeo kama zawadi.
 
Kwa kuwa na wewe upo ili upate uteuzi?
Tulia endelea kuisoma namba awamu yenu imeondoka na mwendazake
 

Kila mtu atimize wajibu wake alipo, ili kutumikia nchi. Rais atateua wangapi? Uongozi wa umma hasa nafasi za uteuzi haziombwi. Ukiona mtu anaomba kuteuliwa kama vile anaomba zabuni ya biashara huyo hafai.

Moja ya mambo ambayo Mwalimu Nyerere alifanikiwa; ni kujenga miiko na maadili ya uongozi. Ukiteuliwa watu wanajua utatumikia nchi na watu wake siyo kufurahia magari ya kifahari na mshahara. Sikuizi mtu akiteuliwa tunasema, "Junior kaula!" Ndiyo mawazo ya kuomba vyeo.. Tuziache mashine za nchi zimpe Rais watu wa kumsaidia. Na hata hao wanao lobby wakikosa vyeo hawatafanya chochote.
 
Hii culture ya kufikiria kuteuliwa nafasi serikalini ni kupata ulaji ni mbaya na ni dalili ya ufisadi, wenzetu wanaona kuteuliwa ni mzigo maana unafikiria jinsi kazi itakavyokuwa nzito, kuacha business kutumikia uma na kuishi kwenye macho ya jumuiya kila siku, ukipata cheo fanya kazi yako kwa bidii rekebisha kero za wananchi,vyeo ni vitu vya kupita na sio sehemu ya kutengeneza utajiri,kama unataka utajiri kaanzishe kampuni yako sio vyeo vya serikali
 
Waache kusubiria uteuzi wakafanye kazi zozote .....za kujiajiri
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…