Uzalendo wa Kitanzania
JF-Expert Member
- Mar 8, 2020
- 3,585
- 8,106
Rais Samia Ili kuongeza ufanisi teua naibu Waziri Wakuu 3, patia mikataba ya utendaji kazi ya mwaka 1, watakaoshindwa weka pembeni
Wadau hamjamboni nyote?
Huu ni ushauri kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan kuteua Manaibu Waziri Wakuu watendaji 3 badala ya mmoja aliyepo sasa.
Manaibu Waziri Wakuu hao:
Wapatiwe mikataba ya kiutendaji kazi ya mwaka mmoja kutekeleza malengo watakayopangiwa na kuafiki kuyatekeleza.
Watafanyiwa tathmini ya awali ya utendaji ndani ya miezi sita na tathmini ya pili baada ya kuhitimisha mwaka mmoja.
Tathmini hiyo ya kiutendaji ndiyo itaamua kama waoendekee kushika nyadhifa zao au wateuliwe wengineo badala
Wafanye kazi za kiutendaji kama walivyo watendaji wengineo kwenye mashirika au taasisi mbalimbali.
Wapangiwe maeneo ya kusimamia kimkakati kama itakavyoamuliwa kwa kuzingatia umuhimu wa sekta.
Nina uhakika Manaibu hao watafanya kazi kwa kutambua wataendelea na nyadhifa zao kwa sharti la kufanikisha malengo husika.
Ieleweke kuwa Mikataba ya utendakazi kazi ina manufaa ikiwemo kuongeza ufanisi, kuondoa uzembe, kuimarisha uwajibikaji kwa kuzingatia malengo husika na huongeza motisha kiutendaji.
Mheshimiwa Rais ninauhakika mfumo huo utakuwa na matokeo mazuri sana kwenye uchumi wetu.
Karibuni tujadili
Niwatakie usiku mwema