Influenza
JF-Expert Member
- Jul 1, 2018
- 1,509
- 3,756
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hasan anatarajia kuhudhuria Mkutano wa 44 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) utafakaonyika tarehe 17 Agosti 2024 mjini Harare, Zimbabwe.
Rais Dkt. Samia anatarajia kuondoka chini leo tarehe 15 Agosti, 2024 kuhudhuria Mkutano huo wenye kauli mbinu: "Kukuza ubunifu ili kufungua fursa za ukuaji wa uchumi na maendeleo endelevu kuelekea SADC yenye viwanda".
Katika Mkutano huo, Rais Dkt. Samia anatarajia kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Asasi ya Siasa, Ulinzi na Usalama ya SADC akipokea kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Zambia Hakainde Hichilema anayemaliza muda wake.