Rais Samia, Kwanini unabagua dhambi za kukemea?

Bila bila

JF-Expert Member
Joined
Dec 20, 2016
Posts
22,168
Reaction score
39,118
Jana nimekusikiliza vizuri wakati ukihutubia Baraza la Wanawake Waislamu. Dhambi iliyokukera zaidi na kuikemea katika kusanyiko Hilo la Dini ni "Kutukana" (matusi). Dhambi hii ukiigeuza katika makosa ya kijinai ni kosa dogo la kutoa lugha ya matusi ambalo adhabu yake ni faini au kifungo Kati ya miezi 6-12.

Dini mbili kubwa katika nchi hii unayoongoza wewe ni Uislamu na Ukristo. Ukristo umeainisha rasmi makosa 10 ambayo yakiwekewa "Amri" katika vitabu vYao vitakatifu yasitendwe na atakayetenda atastahili hukumu. Uislamu pia unayatambua makosa hayo na kwenda mbali zaidi Kwa sababu Dini hii inajinasinisha kwamba msingi wake ni Upendo.

Niseme Wazi nimeshangazwa na jinsi ulivyochagua kuua Sisimizi wakati kitanda chako kimejaa Nge na Tandu. Hivi kweli Mheshimiwa huoni wala husikii malalamiko ya watu kutekwa, kuteswa, kupotea na wengine kuokotwa tayari wakiwa maiti? Mbona tumeambiwa umechangia Milioni 35 za matibabu ya kijana aliyeokotwa Katavi baada ya kutekwa Dear es salaam? Yaani hata hili ambalo Watanzania wengi wanalijua na wewe mwenyewe umeshiriki bado hukuona umuhimu wa kukemea? Au tuwaamini wanaosema na wewe unawajua Wasiojulikana?

Jambo la pili ni Ushoga. Najua kuna kijana kafungwa Tukuyu Kwa kutamka kwamba aliyeko kwenye picha aliyochora ameshindwa kupiga vita Ushoga. Tuachane naye labda alikuwa anajaribu bangi ikampitosha, lakini mbona kuna Mteule wako uliyempiga chini mwezi uliopita bado anatamba mitaani lakini huyu "Mvuta bangi" wa Kawetere kesi yake imepelelezwa masaa 6, kesi ikaendeshwa dakika 30 na hukumu ikasomwa Kwa dakika 13? Hapa Napo unataka tumuamini huyu Bangi Mtu kwamba kweli umeshindwa kukemea Ushoga na Ufiraji?

Hapana mheshimiwa, Mimi siamini kwamba unabagua watu wa kukushauri. Kwamba wakikushauri "watoto wako" ndo ushauri sahihi lakini wakiongea waumini wenzio unaachana nao? Kwamba hawa waliokushauri kwamba Wafanyabiashara wa Kariakoo walikuwa hawajui Kwa nini wanagoma ndo washauri sahihi kwako Kwa vile wamekuambia ulichotaka kusikia? Kwamba Malalamiko 7 waliyoandika na kupeleka kwenye kikao cha Mawaziri watatu (Fedha, mipango na Biashara) walikuwa hawayajui?

Nimalizie Kwa kusema wewe kama kiongozi wetu tunao wajibu wa kukuheshimu na kukutii, lakini pale tunapoona hujafanya vizuri tunakushauri urekebishe. Tafadhali mheshimiwa matusi ni kitu kidogo Sana kuliko uhai wa watu unaowaongoza. Ukiendelea kupambana na vijiti (matusi) vinavyoelekezwa kwako na kuacha kukemea risasi zinazoelekezwa Kwa watu wako utaonekana mbinafsi na mwisho wa siku utadharaulika. Kitu ambacho Kwa kiongozi si kizuri.
 
Kama bado unamshangaa huyu mtu akili yako ni ndogo sana, speech zake tokea siku ya kwanza zinamuonesha ni mtu wa namna gani na jinsi anavyokosolewa badala abadilike anazidi kutoa speech ambazo watu wanamuona dhaifu,
Mimi sijui kitu kuhusu siasa wala uongozi ila naona mapungufu mengi kwenye hotuba zake ambayo hayambebi kwenye uchaguzi ujao, mama akichagua maneno ya kuongea na speech zake zikawa za kuvutia vitambeba sana uchaguzi ujao ila ndo hivo naona wanamuharibu siwajui ni kina nani

Tafadhali mama naomba uniajiri niwe mshauri wako wa maneno ya kuongea wakati wa speech muhimu ambayo watanzania wengi wanapenda kusikia.
 
Hivi kweli Kwa kuangalia mada niliyoweka inaonekana Nina akili ndogo eti?
 
Kama bado unamshangaa huyu mtu akili yako ni ndogo sana, speech zake tokea siku ya kwanza zinamuonesha ni mtu wa namna gani na jinsi anavyokosolewa badala abadilike anazidi kutoa speech ambazo watu wanamuona dhaifu,
Mimi sijui kitu kuhusu siasa wala uongozi ila naona mapungufu mengi kwenye hotuba zake ambayo hayambebi kwenye uchaguzi ujao, mama akichagua maneno ya kuongea na speech zake zikawa za kuvutia vitambeba sana uchaguzi ujao ila ndo hivo naona wanamuharibu siwajui ni kina nani

Tafadhali mama naomba uniajiri niwe mshauri wako wa maneno ya kuongea wakati wa speech muhimu ambayo watanzania wengi wanapenda kusikia.
Wewe kazi yako kupiga kura, sio kuhesabu na kutoa matokeo, yaani vikaratasi ndio vikitoe chama dume madarakani?
 
Jana nimekusikiliza vizuri wakati ukihutubia Baraza la Wanawake Waislamu. Dhambi iliyokukera zaidi na kuikemea katika kusanyiko Hilo la Dini ni "Kutukana" (matusi). Dhambi hii ukiigeuza katika makosa ya kijinai ni kosa dogo la kutoa lugha ya matusi ambalo adhabu yake ni faini au kifungo Kati ya miezi 6-12.
Dini mbili kubwa katika nchi hii unayoongoza wewe ni Uislamu na Ukristo. Ukristo umeainisha rasmi makosa 10 ambayo yakiwekewa "Amri" katika vitabu vYao vitakatifu yasitendwe na atakayetenda atastahili hukumu. Uislamu pia unayatambua makosa hayo na kwenda mbali zaidi Kwa sababu Dini hii inajinasinisha kwamba msingi wake ni Upendo.
Niseme Wazi nimeshangazwa na jinsi ulivyochagua kuua Sisimizi wakati kitanda chako kimejaa Nge na Tandu. Hivi kweli Mheshimiwa huoni wala husikii malalamiko ya watu kutekwa, kuteswa, kupotea na wengine kuokotwa tayari wakiwa maiti? Mbona tumeambiwa umechangia Milioni 35 za matibabu ya kijana aliyeokotwa Katavi baada ya kutekwa Dear es salaam? Yaani hata hili ambalo Watanzania wengi wanalijua na wewe mwenyewe umeshiriki bado hukuona umuhimu wa kukemea? Au tuwaamini wanaosema na wewe unawajua Wasiojulikana?
Jambo la pili ni Ushoga. Najua kuna kijana kafungwa Tukuyu Kwa kutamka kwamba aliyeko kwenye picha aliyochora ameshindwa kupiga vita Ushoga. Tuachane naye labda alikuwa anajaribu bangi ikampitosha, lakini mbona kuna Mteule wako uliyempiga chini mwezi uliopita bado anatamba mitaani lakini huyu "Mvuta bangi" wa Kawetere kesi yake imepelelezwa masaa 6, kesi ikaendeshwa dakika 30 na hukumu ikasomwa Kwa dakika 13? Hapa Napo unataka tumuamini huyu Bangi Mtu kwamba kweli umeshindwa kukemea Ushoga na Ufiraji?
Hapana mheshimiwa, Mimi siamini kwamba unabagua watu wa kukushauri. Kwamba wakikushauri "watoto wako" ndo ushauri sahihi lakini wakiongea waumini wenzio unaachana nao? Kwamba hawa waliokushauri kwamba Wafanyabiashara wa Kariakoo walikuwa hawajui Kwa nini wanagoma ndo washauri sahihi kwako Kwa vile wamekuambia ulichotaka kusikia? Kwamba Malalamiko 7 waliyoandika na kupeleka kwenye kikao cha Mawaziri watatu (Fedha, mipango na Biashara) walikuwa hawayajui?
Nimalizie Kwa kusema wewe kama kiongozi wetu tunao wajibu wa kukuheshimu na kukutii, lakini pale tunapoona hujafanya vizuri tunakushauri urekebishe. Tafadhali mheshimiwa matusi ni kitu kidogo Sana kuliko uhai wa watu unaowaongoza. Ukiendelea kupambana na vijiti (matusi) vinavyoelekezwa kwako na kuacha kukemea risasi zinazoelekezwa Kwa watu wako utaonekana mbinafsi na mwisho wa siku utadharaulika. Kitu ambacho Kwa kiongozi si kizuri.
Rais wetu ni marufuki kukemea ushoga
 
Back
Top Bottom