Pre GE2025 Rais Samia: Mnashuhudia matusi ninayotukanwa lakini sijibu najigeuza chura

Pre GE2025 Rais Samia: Mnashuhudia matusi ninayotukanwa lakini sijibu najigeuza chura

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Nyendo

JF-Expert Member
Joined
Jun 4, 2017
Posts
1,336
Reaction score
4,731
Na mimi kazi mliyonipa nasimama na ninaifanya na mnashuhudia matusi ninayotukanwa mpuuzi, hana maana, huyu Bibi ana hivi, mambo tele lakini najigeuza chura.

Kwahiyo nyingi zinapigwa kelele wakiona haujibu sasa tulitukane litajibu ama halijibu, sijibu nageuza chura masikio sisikii kabisa, ninachotaka mageuzi ya kiuchumi ndani ya nchi hii sitaki kingine sasa kwenye mageuzi haya tutakanyaga nguru wa mshihiri, anayetaka kunikera na mimi anikanyagie uchumi wangu,"


===

Pia soma:

 
Ingawaje kuna tofauti kati ya kuwa kiziwi na kujifanya kiziwi! (To pretend)
Wanasema pretenders are worse than murderers.
 
Rais kuzungukwa na watu feki sana. Hayati mzee mkapa kwenye kitabu chake ameliongelea hili. Kuwa kipindi akiwa raisi, kulikuwa na genge la watendaji ambao alipokuwa akikosea wao walimpa uhakika tena wa juu kuwa yupo sahihi na ashikamanie maamuzi hayo hayo ila baada ya kutoka watu hao hao ndio walimsema kuwa yeye ndie aliyetaka mambo yawe hivyo, meaning ni kwamba mzee mkapa aliona tatizo live bila chenga kuwa kuna watu wapo serikalini hawana mamlaka ila ndio genge la ushawishi ambalo hushawishi maoni yao yawe kipaumbele ili waweze kupata chochote kitu.

Kimsingi bi mkubwa hajastuka. Mshahara mkubwa, kila mtu anakupa sifa, kila kona ni mapambio, kelele za wanaichi anaambiwa kuna upinzani nyuma yao so awapuuze, ratiba za kupangiwa kusafiri bila utaratibu, watendaji masnitch na wachumia tumbo, kukaa mbali na MUNGU na kujiweka karibu na miungu watu, kuzungukwa na matajiri ambao ni wepesi sana kumpa zawadi za pesa nyingi sana matokeo yake wanafanya ajione ana bahati na amezungukwa na marafiki kumbe hakuna kitu hawa wote huwa wanakimbia baadae akishamaliza uraisi.
 
Back
Top Bottom