Rais Samia: Msiseme Mama anazunguka tu, sitozunguka bila sababu

watanzania ni lawama tu,,mlisema amekaa nje ya nchi na ofisini..etu hatembelei wananchi..leo kafanya ziara ya sikutatu mohi na arusha .mmebaki kulalamika hivi nyie mkoje.Mbona magufuri alikuwa nakyembelea wananchi na convoy kubwa
Hakika mkuu 😍
 
Usichokijua ni kuwa mradi wa maji alioutembelea eneo la Chekereni utamaliza tatizo la maji ndani ya jiji la Arusha kwa asilimia kubwa sana, thamani ya mradi ni mabilioni ya fedha, bado ametembelea hospital ya serikali iliyopo eneo la Njiro iliyojengwa kwa mamilioni ya fedha, miradi mikubwa kama hii ni vizuri ikipata attention ya raisi mwenyewe maana inaipa uzito wa aina yake.

Hilo la kina Bananga ni chumvi katika mboga iliyojaa nyama nyingi, mafuta ya kula, nyanya, vitunguu aina zote pamoja na vikorombwezo vya kila aina kwa mapishi wa nyama (Siasa).
 
Pingapinga fc kazini

Akienda nje anazurula nje hajali wananchi wake, akipokea wageni ikulu mvivu anakaa tu ofisini, akitembelea wananchi na kuzindua miradi ya maendeleo anazunguka tu

Nakushauri tu ndugu! Chuki zako dhidi ya Mama Samia zitakuua

Tafuta kazi ya kufanya Au ukishindwa ndimu ziko nyingi tengeneza juice unywe
 
Pingapinga FC🤣
 
Kwani hata asinge tembele huo mradi nini kingetokea.. weka hoja nyingine hii ni utoto ..
 
Umenena kiongozi, yaani watz tunachanganya mno na mambo km haya ndo hufanya akitokea kiongozi mwenye kibri basi yanampa mwanya wa kujiamulia na kujiachia tu kwa jinsi yoyote anayotaka maana anajua watu wenyewe nao ni chenga tu
 
Umenena kiongozi, yaani watz tunachanganya mno na mambo km haya ndo hufanya akitokea kiongozi mwenye kibri basi yanampa mwanya wa kujiamulia na kujiachia tu kwa jinsi yoyote anayotaka maana anajua watu wenyewe nao ni chenga tu
Umeongea jambo adhimu sana !
 
Leta hoja ziara ya hangaya ina faida gani kwa taifa?
Nimeshaandika kwa kirefu huko juu...

1)MRADI WA MAJI CHEKERENI(BILIONI 520)

2)KIWANDA KIKUBWA CHA NYAMA KARIBU NA NAMANGA

Unataka RAIS asihudhurie zinduzi/funguzi hizo ilihali ni eneo mojawapo la kukutana nasi wananchi?!!!
 
Kwani hata asinge tembele huo mradi nini kingetokea.. weka hoja nyingine hii ni utoto ..
Mfano mwepesi wa kitoto, umeotesha miche yako mahali na ukawaachia watoto wamwagilizie then wajue kuwa kamwe hutakuja tembelea eneo la tukio, sidhani kama utapata unachotarajia. Raisi ni kama Mama/ Baba wa Taifa. Hii ipo Tanzania, Africa, Ulaya, America mpaka Asia… we wa wapi? Raisi sio kukaa ofisini pekee…
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…