kevylameck
Member
- Nov 3, 2013
- 18
- 19
Miongoni mwa yasiyopimika kwenye mizani ya namna yeyote ile ni athari kubwa ya SAMIA SULUHU HASSAN kwa wasichana wadogo na mabinti.
Dkt. Samia Suluhu si tu ni Rais wa Tanzania lakini pia ni Mwanamke wa kwanza kuwa Mkuu wa serikali na Mwenyekiti wa Chama Tawala - CCM.
Katikati ya mashaka ya wengi waliokuwa wameathiriwa awali na mfumo dume, Leo Dkt. Samia ni Lulu na kielelezo kikuu kwa wadogo zetu.
Muulize mtoto wa kike hii leo anatamani kuwa nani baadae- Majibu yake linganisha na majibu ya miaka ya nyuma ama simulizi zozote ulizowahi kuzisikia hapo kabla.
Edna Lameck, Katibu wa Hamasa na Chipukizi UVCCM katika moja ya mazungumzo naye anasema Rais Samia amekuwa mfano wa pekee na ameongeza ujasiri mkubwa kwa watoto wa kike katika kuamini ndoto walizo nazo.
Edna akanikumbusha mfano wa wanafunzi waliowahi kuulizwa masomoni kwamba wanatamani kuja kuwa kina nani ukubwani.
Mtoto wa kiume yeye akasema anatamani sana kuwa Rais wa Nchi - Mtoto wa kike yeye akasema anatamani kuwa Mke wa Rais.
Mfano huu ndicho kilichokuwa kimesalia vichwani mwa mabinti wengi wa zama hizo. Hawakuona upenyo wowote wa wao kushika nafasi za juu za kimaamuzi.
Mifumo dume iliyokita mizizi ikisindikizwa na harakati za kumdogosha mwanamke zilikuwa ni shimo lililomeza ujasiri wao.
Miaka chini ya 70 hii leo tangu nchi nyingi za Afrika zipate uhuru kama asemavyo Edna Lameck, nami nakiri kuwa Samia ni mchochezi wa ndoto za watoto wa kike.
Samia Suluhu Hassan ni kielelezo cha juu kabisa cha kupigiwa mfano kuwa Mabinti wa Kitanzania wanaweza kufika juu kabisa kwenye nafasi za maamuzi kama ilivyo kwa wanaume.
Mfano dhahiri wa hamasa aliyoitia kwenye mioyo ya mabinti wengi ni tukio la May 18 mwaka huu. Tulishuhudia mtoto Georgina Magesa akiruhusiwa kuketi kwenye kiti cha Rais Samia wakati wa uzinduzi wa minara ya Azam Tv.
Rais Samia alifikia hatua hiyo baada ya kuona makala fupi ya Georgina, ikimuonesha akieleza ndoto zake za kutamani kuwa Rais wa Tanzania kwa siku za mbeleni.
Mfano mwingine ni tukio kubwa la juzi ambalo limeandikisha historia mpya kwa nchi yetu na kusisimua tena ndoto za wasichana wengi wa kitanzania kama sio Afrika nzima.
Nimeshuhudia kwenye runinga Rais wetu Dkt. Samia akimpokea mwanamke mwenzake Mh. Katalin Novàk ambaye ni Rais mdogo zaidi kiumri na wa kwanza mwanamke kwa taifa la Hungary.
Ni mara ya kwanza kwenye ardhi ya nchi yetu kushuhudia Marais wawili wa kike kwenye nchi zao wakiwa Ikulu yetu ya Magogoni.
Dhahiri ambayo bila shaka hutoweza kubishana nami ni kuwa katika karne hii, tutashuhudia mabadiliko makubwa ya uongozi na mtazamo wa jamii kwa mwanamke.
Bahati nzuri zaidi ni kwamba kuanzia ripoti za Forbes (2021) mpaka macho yetu yanachochea mitazamo hiyo kutokana na matokeo chanya ya wanawake walio kwenye uongozi wakiongozwa na Rais Samia.
Kama ifanyavyo Idara ya Chipukizi wa UVCCM naamini kabisa mimi na wewe tunalo jukumu la kubadilisha mitazamo yetu kuhusu wanawake na kuendelea kukuza, kuhifadhi na kutunza ndoto hizi za watoto wa kike na wadogo zetu.