Rais Samia, nakuomba angalia upya Mradi wa BRT Dar

Tatizo viongozi wetu hawasafiri, huyo “kipenzi chetu “ Magufuli aliishia Burundi tu, na hata wakisafiri hawatembei! Mtu mwenye uzoefu wa kuishi nje ya nchi hasa za Ulaya na America kwa muda mrefu ndio anaweza kuleta mawazo mazuri sio hawa viongozi wetu wa Dar-Dodoma.
 
Naunga mkono hoja
 
Hapana wanasafiri sana ila sisi hatuwezi jua. Mara nyingi wanafanya safari za kitalii. Hapo ndipo wana kuwa na uwezo wa kutembelea sehemu nyingi private na.kujionea mambo mengi jinsi yalivyo kwenye nchi za wwnzetu.

Tatizo kubwa ninalo liona ni kuwa wanakosa maarifa mapana kama ya Hayati Rais Magufuli. Lile jamaa liliipenda Tanzania na watanzania kwa ujumla. Alikuwa yuko tayari kufa kuliko kuona wananchi wenzake na nchi yake inateseka.

Tanzania tunakosa wanasayansi wanao jiamini. Katika nchi zenye mfumo kama huu wa kwetu ni Rais tu peke yake mwenye uwezo wa kubadilisha hali ya maisha ya nchi. Kama Rais hana vision na uwezo wa ku impliment yale anayo yataka na kuyaona, hiyo sahau.

Viongozi wengine wote hawawezi kufanya mambo wanayotaka bila Rais kutia idhini yake ya kutoa pesa za ku finance mambo hayo wanayo taka yafanyike.

Kitu kikubwa kinacho tuharibu ni kule kukosa spirit ya uwajibikaji wa watendaji wizarani na kwenye taasisi zinazohusika na utekelezaji wa malengo na maazimio ya serikali. Watumishi wanaopewa madaraka mara nyingi huwa hawatendi yale mambo kama ilivyo kusudiwa.

Hizo hela za miradi kutoka serikali kuu na halmashauri watumishi na watendaji always wanazipigia mahesabu jinsi gani wao binafsi wataweza faidika na hela hizo za miradi ya maendeleo. Hapo haijalishi kama hana barabara ya kupita na gari lake au la. Anacho taka ni hela mfukoni ili aonekane kwa watu kuwa yeye ni tajiri na kuzifanyia hizo hela matumizi ya mambo ya hanatha.
 
Niambie basi anachoigiza ili na mimi niweze kutoa mchango wangu juu ya maigizo yake.

Mimi kila mwaka nakuwa Bongo mara mbili kwa mwaka kwa kipindi cha miezi miwili mpaka mitatu. Mda unao bakia nakuwa Europe.
Hongere mkuu nipe na mimi mchongo nije huko nioshe macho kidogo
 
Hongere mkuu nipe na mimi mchongo nije huko nioshe macho kidogo
[emoji16][emoji16][emoji16]Ningekushauri baki tu Tanzania na ijenge Tanzania yetu. Mbona Tanzania ni nchi nzuri sana! Europe ni stress pure! Ulaya kwa wewe mtu mweusi utakuwa mtumwa tu ndugu yangu bila kujitambua. Mimi nina miaka 35 Ulaya, lakini kwenye nchi ninayo ishi wananiona ni "Alien" tu. Hata nifanye nini ninabaki kuwa Alien kwao. Ni kitu ambacho kina ninyima raha sana. Ndiyo maana huwa nakuja ku Tank furaha Tanzania.
 
Commutter trains (London) na tramways (Warsaw) na mwendokasi (Dar, Dubei, Bogota na Bangkok) ni kitu hichohicho kimoja: concept ni kwamba yawe na exclusive right of way kwenye njia yake, yasiwe na foleni. Hayo matatizo au fursa unazosema ni hizohizo across the board. Latest research indicates that "BRT" ya buses au trams au trains zote ni mwendokasi. Ipi uchague ni gharama ya magari (light metals, aluminium) na train/tram ambazo ni chuma tupu

Kuhusu pollution, dawa yake na CNG, compressed natural gas, sasa hii most motor vehicles are converting to CNG while some manufacturers (Honda, Volvo, Samsung, Ikarus) are already manufacturing for CNG fuel.

Cha kufanya ni tuwape support mwendokasi wasambae mji mzima, then wahamie Zanzibar, Mwanza, Mbeya, kote.

Tatizo kubwa linalotajwa ni mtaji, kwa private sector, au bajeti ya serkali. Hili nalo tayari lilishatuliwa - tutatumia soko la hisa DSE kupata collective investors. Mwendojasi itaunganishwa na terminals kuwa na shopping malls kama za Dubai na Thailand. Kwa kutumia kitu huitwa REITS (real estate investment trusts) tutabadilisha kabisa mfumo mzima wa infrastructure funding na mfumo wetu wa fedha.
 
Mkuu mimi nachotaka ni pesa, issue ya heshima hiyo kwangu haina nafasi, hata wanione kinyesi poa tu.
 
UDART panakosekana uongozi na utaalam wa kuendesha shirika la usafirishaji kisasa. Serikali ingerudisha Public Private Partnership(PPP) ili UDART ijiendeshe kama entity ya kibiashara. Kuanzia maintenance ya mabasi, maintenance ya mifumo iliyofungwa, usimamizi wa vituo, usimaizi wa route, kukusanya nauli/mapato ni vitu vinaweza kuvunjwa vikafanywa na private entities ziwe na SLA za kuwawajibisha. UDART abaki kufanya supervision, kulipa mishahara na kuangalia maslahi ya serikali na shareholders wengine.

Phase 1 hii cha mtoto, nasubiri kuona Phase 2 huko mbagala ile nyomi kwa style hii ya ubabaishaji watafanyaje.
 
Mkuu mimi nachotaka ni pesa, issue ya heshima hiyo kwangu haina nafasi, hata wanione kinyesi poa tu.
[emoji1787][emoji1787][emoji1787] Duh! Sawa kwa msimamo wako thabiti! Lakini elewa kuwa hata ukipata nafasi ya kwenda kufanya kazi na kuishi Ulaya utataka kuwa na familia ambayo hiyo ndiyo itapata shida sana baadae na manyanyaso ya wazungu.

Kumbuka pia kuwa wewe sio ndiyo uliyeanza kuwa na fikra hizo, hata sisi tulipokuwa tuko Bongo kabla ya kwenda Ulaya tulikuwa na mawazo hayo hayo, lakini ukisha isha nao kwa mda mrefu na umri ukikuingia kidogo ndiyo hapo unaona "majuto ni mjukuu." Unaanza kuona athari ulizozipata mpaka kwenye familia yako.

Inaumoza sana. Na inavunja moyo. Nikutakia mafanikio makubwa katika jitihada zako za kqenda kutafuta hela Ulaya au Amerika..
 
Daladala zirejeshwe tu njia ya ferry, Posta, fire,magomeni, manzense, ubungo,kimara na mbezi ndio ujinga wa kuendesha Mwendokasi kupumbavu utakoma kujaza gani kule
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…