Rais Samia naomba ushughulikie Malipo ya Wastaafu Kiwanda cha Karatasi Mgololo

Rais Samia naomba ushughulikie Malipo ya Wastaafu Kiwanda cha Karatasi Mgololo

mtwa mkulu

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2013
Posts
8,586
Reaction score
11,227
Mh. Rais, kiwanda cha karatasi kilichopo wilaya ya Mufindi mkoa wa Iringa kiitwacho Mufindi paper mills LTD (MPM) zamani Southern Paper Mills (SPM) kilichokuwa kinamilikiwa na Serikali ya Jamhuri ya Tanzania 100%, chini ya shirika la Maendeleo la Taifa (NDC), kwasasa kinamilikiwa na kampuni ya Rai Group Limited ya nchini Kenya.

Kiwanda hiki cha Mgololo kilianzishwa rasmi na kuzinduliwa na Rais wa kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, hayati Mwl. Julius. K. Nyerere mwaka 1985 kikiwa na thamani ya Bilioni Tano za Kitanzania kwa wakati huo, jukumu lake kuu ilikuwa kuzalisha karatasi kwa kutumia malighafi za ndani toka katika msitu wa Saohili Mafinga, lengo ilikuwa ni kufanya biashara na kuongeza wigo wa ajira kwa watanzania.

Na kukazia hilo, Mwakimu Nyerere aliamua kujenge shule ya ufundi Ifunda Tech maalumu kwaajili ya kuzalisha wataalamu mbalimbali wa kuendesha kiwanda hicho, sawa kabisa na Arusha Tech iliyokuwa shule kwaajili ya kuwanda cha Arusha tools.

Tarehe 24/01/1997 kwa waraka wa Serikali (Government Notes) namba 33, Serikali ili-specify Kiwanda na kukiweka chini ya tume ya kurekebisha mashirika ya umma (PSRC) iliyopewa jukumu la kusimamia shughuli za Kiwanda zikiwemo huduma kwa wafanyakazi wanaotunza kiwanda kwa kufanya uzalishaji mdogo mdogo (mill warming) na pia kutafuta mwekezaji (kukinadi hatimaye kukiuza kiwanda).

Tarehe 13/02/2004 kiwanda kilikabidhiwa rasmi kwa Rai Group ya Kenya kwa maelezo ya kuwa wao ndio wanunuzi wa Kiwanda hicho adimu barani Afrika, hakuna taarifa rasmi za bei ya ununuzi wa kiwanda hicho lakini inatajwa kuwa kiliuzwa kwa Tsh. bilioni moja za Kitanzania.

Mh. Rais, baada ya kiwanda hiki kubinafsishwa. Muwekezaji aliongeza muda wa kazi kuwa saa 24 huku kazi zikifanyika weakend na siku za sikukuu. Aidha hakukuwa na nyongeza ya mishahara jambo ambalo watanzania hawa wazalendo hawakulizoea. Ikumbukwe kuwa kiwanda wakati huo kilikuwa na wafanyakazi zaidi ya 1000 wenye afya njema na weredi.

Mh. Rais, Watanzania wenzako hawa walilazimika kuingia katika mgomo mkubwa kwa mujibu wa sheria mara baada ya mazungumzo na serikali na muajili kushindikana. Mgomo huu nakumbuka uliingiliwa kati na muhimili unaouongoza kwa kumtuma mtu wa uwekezaji mama palangyo ambaye alifungiwa kiwandani.

Baadaye muhimili wako ulituma askari zaidi ya 300 wenye siraha za moto kupiga wafanyakazi hao, kuwa vunja viungo na kusababisha vifo viwili siku hiyo japo vilitokea nje ya mgololo. Askari wako wahuni wakimtetea muhindi waliwasha kiwanda kwa mabavu na kuweka ulinzi zaidi ya miaka mitatu baadae. Ukatili huu watanzania walifanyiana kwenye ardhi ya Mwalimu.

Mh. Rais, baada ya mgomo huu serikali yako iliridhia kufukuzwa kazi kwa zaidi ya wafanyakazi 900 ambao walikatiwa umeme na maji, wakafukuzwa mgololo wengine na kuingia kwenye maisha magumu, mpaka sasa zaidi ya 300 wamekufa vibaya kutokana na hali ngumu iliyo wakumba.

Mh. Rais, wazee hawa walikubali yote waliyofanyiwa na serikali dhalimu. Ila waliingia mahakamani kuomba lau mafao yao halali waliyotumikia kwa miaka mingi. Lakini hata hivyo walizungushwa mpaka mwaka 2017 muajili mpya alipo walipa mafao kiduchu kwa muda mchache walio mtumikia.

Mh. Rais, Serikali yako imeendelea kuwakandamiza wazee hawa kwa kukalia mafao yao. Tangu mwaka 2006 mpaka leo wapo kwenye kesi isiyo na ukomo. Baadhi yao viongozi wao wamenusurika hata kuwekewa sumu ili wafe kelele zipungue.

Mh. Rais, nakuomba kwa mara ya mwisho sitaomba tena, uwalipe wazee hawa. Endapo utakaidi sisi tutaendelea kuwazika tuu wazee hawa kama viazi ila kumbuka damu yao itazaa matunda ya ukombozi kwa taifa lao hili.

Natanguliza shukrani

MTWA mkulu

IMG-20230414-WA0004.jpg
 
Kwa nini Rais ashughulikie na sio katibu mkuu, waziri wa wizara husika au waziri mkuu??
 
Kwa nini Rais ashughulikie na sio katibu mkuu, waziri wa wizara husika au waziri mkuu??
Wanalo hilo file kila siku wanaperuzi kama gazeti la uwazi
 
Makonda amesema angemtia leo makofi Naibu waziri hii issue
 
Hii nchi ngumu sana tangu zamani.
 
Back
Top Bottom