PostGE2025 Rais Samia: Nawapongeza Wanzanzibar, Tumefanya uchaguzi hakuna aliyenyukuliwa

Conversations and stories after Tanzania's 2025 General Elections

Mawele

Platinum Member
Joined
Jul 25, 2023
Posts
1,161
Reaction score
4,251
Aliyeshinda kapewa aliyeshindwa kasema asante’

Your browser is not able to display this video.

​
"Jambo jingine ninalotaka kuzungumza ninyi ni kulinda amani na utulivu wa nchi yetu.

Nawapongeza na kuwasalimu Wazanzibari mwaka huu. Tumefanya uchaguzi hakuna aliyenyukuliwa, yupo? Tumekwenda, tumefanya kwa amani na utulivu, sivyo? Tukijua sote ni Wazanzibari, sivyo?

Haya, aliyeshinda kapewa, aliyeshindwa kasema asante. Tumekaa, tunajenga... mniambie msani pale Mkulima nchi inakwenda, sivyo? Sasa hivi ndivyo inavyotakiwa Wazanzibari tuishi. Sisi wote ni wa nani? Wa nchi hii, wa kisiwa hivi, na lazima tuishi pamoja kwa maendeleo yetu.

Kwa hiyo kushindana kumwacha Simba na Yanga si wanashindana? Tena ushindani mkubwa, sio? Tena tunawapongeza kesho wanakuja kufanya dabi hapa Kuunga... Wanakuja kuunga Kizimkazi Festival, sio? Dabi kesho linapigwa Zanzibar hapa. Sasa hata wale tukiwa Simba na Yanga na sare zetu hapa, si tupe Simba na Yanga?

Hiza langu mimi ni kusisitiza tena umoja na mshikamano."
 
Dah!

Maskini Tanzania!
Kawaida huwa sisikilizi video za huyu mtu. Imenilazimu tu leo nisikilize baada ya kusoma yaliyoandikwa.

Kaitengeneza historia kwa njia mbalimbali huyu mwanamke.
 
Kunyukuliwa maana yake nini ?
 
Tunaijua hiyo bwana, kumsifia mmoja ili mwingine ajisikie hatia.

A beginner’s weak manipulation tactics, ambazo hazifanyi kazi kwenye siasa, zinafanya kazi huko kwa watoto wa vidudu.
 
98% alishinda!🤭🤭🤭
Kwa kupigiwa kura ya ndio na waTanzania milioni 30 kati ya 31 waliojitokeza kupiga kura..
Sasa watu hao hao waliompenda na kumpa kura nyingi hivyo anawahimiza wafanye maridhiano, sijui na nani na kwa sababu zipi!
Unaweza kusaidia kueleza jibu la mihangaiko yake hii ya kuimba nyimbo za AMANI kila mara?

Watu wanampenda sana huyu, hata hahitaji kuzungukwa na mitutu ya bunduki kila mahali anakokwenda.
 
Mtu unapendwa na watanzania kwa 98% na hapo unaishi kwa kuwaogopa kama digidigi akikohoa mmoja unamfuata chapu unafinya. Unasubiri mwingine akianza kukusifia tu humwamini unapita nae. Tuseme hawa wanaomkosoa ni wanamsifia maana si ndio walipiga kura wakampa kura yeye iweje mkosoe mapema ivi?
 
Zero brain killer
 
Akivuka akirudi bara tu anavuka na makasiriko, chuki, binafsi, choyo...kiufupi atavuka na kisilani akiwakumbuka watanganyika walivyo na midomo mipana😀😀
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…