Rais Samia, neno lako tu litasaidia wakazi wa Mpiji na Makabe kupata Lami

Muite

JF-Expert Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
2,971
Reaction score
6,607
Rais wetu Mpendwa, binafsi najiona mwenye bahati kuwa na Rais wa aina yako. Kikubwa zaidi ni kwa jinsi ulivyoubeba uhusika wa kuwa Kiongozi usiyebagua watu wako. Zaidi ya kuwa Kiongozi wa Taifa letu lakini pia Umejaaliwa SANA UTU.

Mama yetu pamoja na Majukumu mengi uliyonayo natamani japo UMUULIZE WAZIRI WA UJENZI KUHUSU BARABARA ZA MPIJI NA MAKABE. Najua utakapoulizia tu hizo barabara zitajegwa tu.

Nasema hivi kwasababu ndio hulka za watendaji wengi wa nchi yetu kwani wakisikia umeulizia ndipo nao watakapoanza kukimbizana wakiambiana "jamani Mheshimiwa Rais amehoji kuhusu hizi barabara".

MUNGU AKUBARIKA NA AKUJAALIE UPATE WASAIDIZI WENYE KUGUSWA NA MAISHA YA WATU KAMA ULIVYO WEWE
 
Kipind cha Magu hiyo barabara ilikuwa kwenye plan ya kuwekwa Lami. Baada ya hapo sijui nini kimetokea kimya mpaka leo
 
Hii Barabara ya mbezi mpaka bunju B ikijengwa kiwango Cha lami itasaidia sana, wakazi wa mpiji ni kama wametelekezwa. ,Hata usafiri wa uma ni shida ,kwanza waligoma kutokana na ubovu wa Barabara
 
Kama hamkupata barabara wakati wa JPM ndio basi tena, kwasasa zinajengwa chache za kiwango duni.
 
Rais wetu Mpendwa, binafsi najiona mwenye bahati kuwa na Rais wa aina yako. Kikubwa zaidi ni kwa jinsi ulivyoubeba uhusika wa kuwa Kiongozi usiyebagua watu wako. Zaidi ya kuwa Kiongozi wa Taifa letu lakini pia Umejaaliwa SANA UTU.

Mama yetu pamoja na Majukumu mengi uliyonayo natamani japo UMUULIZE WAZIRI WA UJENZI KUHUSU BARABARA ZA MPIJI NA MAKABE. Najua utakapoulizia tu hizo barabara zitajegwa tu.

Nasema hivi kwasababu ndio hulka za watendaji wengi wa nchi yetu kwani wakisikia umeulizia ndipo nao watakapoanza kukimbizana wakiambiana "jamani Mheshimiwa Rais amehoji kuhusu hizi barabara".

MUNGU AKUBARIKA NA AKUJAALIE UPATE WASAIDIZI WENYE KUGUSWA NA MAISHA YA WATU KAMA ULIVYO WEWE
Anaumia na kitu gani mtu anayeishi Magogoni na Masaki? Mbunge wenu kazi yake ni kusifia ufisadi kwa nia ya kupata cheo. Barabara za Makabe, Msumi, Mpji na Mbopo kuendelezwa kwa kiwango cha lami mpaka wananchi mjitoe ufahamu kama suala la DP World maana ni za muda mrefu mno kuahidiwa. Kwenye ilani waliahidi lakini mpaka sasa wametengeneza mita 600 tu kiwango cha lami wakati zinahitajita sio chini ya kilomita 20
 
Of course huyu Mbunge tuliyenaye bwana Mtemvu sio kama wananchi walivyokuwa wanatarajia mambo ya maana kutoka kwake. Kwa kiasi kikubwa wananchi hawana imani naye kabisa maana hata kuonyesha kuwa anapambana kwa ajili ya jimbo hakuna kitu.
Kwa upande wa Mama tunasema kauli yake inaweza kumaliza na kuharakisha hizi changamoto za Barabara na Maji maana ndivyo watendaji wengi walivyolelewa hivyo hapa nchini tangu Uhuru, waziri/Mkurugenzi atafanya jambo pale tu atakaposikia Rais ameulizia. Yaani itokee Mama aulizie sula la Maji na Barabara maeneo hayo UTASHANGAA WATAKAVYOKIMBIZANA KUWEKA MAMBO SAWA.
IMAGINE SASAHIVI WANANCHI WA MAENEO HAYO WANAAMINI SUALA LA MAJI LIMEKUWA HALIFANYIWI KAZI SABABU TU WATENDAJI WA WILAYA NA DAWASA KUFAIDIKA NA HELA ZA WAUZAJI WA MAJI KWA MAGARI
 
Back
Top Bottom