figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,724
- 55,906
Salamu Wakuu,
Ni aibu kubwa kwa Mwanachama wa CCM, kumuita rais wa Nchi ya Tanzania eti ni Mama wa Kizanzibari. Hii ni fedheha kwa chama na Serikali na Taifa kwa Ujumla.
Nchi yetu imejijengea heshima kwa kuheshimiana na kuwa na Usawa, sasa haya Mambo yanatoka wapi?
Wasiwasi wangu ni hawa wafuasi wa Hayati Magufuli kulazimisha Rais Samia afanye kama Magufuli. Rais Samia anafanya kazi kwa manufaa ya Watanzania wote, sio Wafuasi wa Magufuli tu, hata Mumlishe Maneno kwenye Magazeti kwamba hatagombea. Mnampa Ushauri na taarifa za uongo ili aonekane hafai. Mnabambikizia watu kesi ili rais alaumiwe. SAMIA Hatetereki.
Je, 2025 Rais Samia ataweza kushinda Wanachama wa CCM ambao ni Wafuasi wa Magufuli kwa hizi siasa chafu? Sababu hata sasa akiongea hawamsikilizi, Wanaamua watakalo. Wanaweza kuongeza tozo, Kumjibu Makanisani, Mitandao ya kijamii na hawafanywi kitu.
Wakati wenu ushaisha. Tumpe nafasi rais Samia afanye analoweza na mwingine aje afanye analoweza.
Nakutia moyo Rais Samia. Wasikutishe, endeleza kiporo cha katiba mpya. Wanaokutisha wanaogopa kupoteza Ugali wao ndio maana wanasema Katiba mpya haifai.
Nenda nao kwa akili hivyo hivyo.