Pre GE2025 Rais Samia: Nilipomteua Mwana FA na Nikki wa Pili sikueleweka lakini sasa wananisaidia sana

Pre GE2025 Rais Samia: Nilipomteua Mwana FA na Nikki wa Pili sikueleweka lakini sasa wananisaidia sana

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Mindyou

JF-Expert Member
Joined
Sep 2, 2024
Posts
1,869
Reaction score
4,877
Wakuu,

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amepongeza utendaji wa Mbunge wa Jimbo la Muheza ambaye pia ni Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamisi Mwinjuma (Mwana FA), na Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Nickson John Simon (Nikk wa Pili), akieleza kuwa wamekuwa msaada mkubwa serikalini.

Akihutubia wananchi wa wilaya ya Muheza, Rais Samia alisema kuwa uteuzi wa wasanii hao wawili ulizua maswali kwa baadhi ya watu, lakini sasa wameonesha uwezo wao mkubwa wa kiuongozi na kujituma katika majukumu yao.

"Nilipomteua Mwana FA (Hamisi Mwinjuma, Mbunge wa Jimbo la Muheza) na yule Mkuu wangu wa Wilaya ya Kibaha anaitwa Nikk wa Pili (Nickson John Simon) watu hawakuelewa lakini kwa faraja kubwa, hawa wananisaidia sana," amesema Rais Samia.

 
Kumbebesha yule dayaspora mstaafu libendera azunguke nalo huko mikoani na kuimba mapambio ya mama hivi mama vile ndicho kitu pekee alichojua kufanya. Halafu yule dayaspora mstaafu alivyokuwa anavimba kumbe hakuna kitu.
 
KWA KIPI HICHO?Dah panahitajika reform wa ukuu wa nchi.kwa herufi kubwa HATUNA RAIS
 
Back
Top Bottom