Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Rais Samia akizungumza na wananchi wa Peramiho amesema kuwa Sera ya CCM ni wananchi waishi maisha ya amani na kuwe na utulivu wa kisiasa wananchi waweze kufanya mambo yao kwa raha kabisa, hayo mambo mengine waachie wenyewe.
Nendeni mkachague wagombea wa CCM kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa ili tuweze kupanga safu ya kuvuka vizuri kwenye uchaguzi wa 2025 tuweze kuiendeleza Tanzania yetu.
Nitoe wito tuendelee kudumisha amani ,utulivu na usalama katika maeneo yetu. Leo kungekuwa na vurugu huko, wingi wa umati ulio hapa usingekuwepo. Kila mtu angekuwa katafuta sehemu ya kubana ili asitoke kwa kukimbia vurugu, kwa sababu ya amani leo mmekuja kumuona kiongozi wenu kwa wingi namna hii.