Rais Samia Suluhu ajikite kutekeleza ndoto za Hayati Magufuli au atekeleze maono yake?

Rais Samia Suluhu ajikite kutekeleza ndoto za Hayati Magufuli au atekeleze maono yake?

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Je, tunamshauri Rais mpya aendelee na miradi yote aliyoanzisha JPM au aendeleze ile miradi yenye tija kwa Taifa na pia aanzishe miradi ya ndoto zake?

Hapa Kuna miradi yakitaifa na miradi ya maono binafsi ya JPM. Miradi yakitaifa ni mradi wa umeme wa rufiji, mradi wa reli, bomba la mafuta, ujenzi miundombinu ikiwemo umeme na kuboresha utoaji huduma.

Miradi ambayo haikuwa na sura ya kitaifa Ni ile iliyofanyika chako ikiwemo hifadhi,uwanja wa ndege, uwanja wa mpira, mahoteli na ofisi za umma nk

Katika miradi yote hii lazima kwa kauli moja Rais aseme Tanzania ina uwezo mdogo kiuchumi na kwamba nasimama na miradi ya kitaifa na endapo chenchi itabaki ntaangali chato. Asipofanya hivyo akasema anaendeleza kila alichoanzisha mzee JPM tutakwama.

Tumshauri Rais vyema.
 
Unataka atekeleze mambo ya kuteka watu, kukwapua korosho, kukwapua hela za wafanyabiashara, kukanyaga katiba, kuonea wapinzani, kutoa kauli za kukera, kuiba chaguzi, kugeuza vyombo vya habari kuwa vya kusifu na kuimba mapambio, kubambikizia watu kesi za uhujumu uchumi ili kuwakomesha, kununua wapinzani njaa na kuligeuza bunge na mahakama kuwa kama vikaragosi vyake?
 
Ndoto zibaki ndoto tu za aliyeziota Serikali yoyote ya wenye akili haijihusishi nazo maana mara kwa mara nyingi hazina ukweli.

Serikali itekeleze mipango yake yenye manufaa kwa wananchi na iachane na ndoto za mtu binafsi akae nazo au aende nazo kama anaona zitamsaidia mbele ya safari.

Tumeona miaka 6 Serikali imekuwa inahangaika na ndoto kwa gharama kubwa lakini matokeo yake yanasemwa tu hayaonekani badala yake inaonyesha Miradi iliyokamilika au inaendelea kutekelezwa ya Serikali zilizopita.

Bwawa la Umeme na ATC na Dodoma kuwa Mji Mkuu ni Miradi ya Awamu ya Kwanza, Flyovers na DRT na SGR na Salendar Bridge Awamu ya Nne, na mingine mingi. Miradi ya Chato wanaijua na kuiona wa huko.
 
Je, tunamshauri Rais mpya aendelee na miradi yote aliyoanzisha JPM au aendeleze ile miradi yenye tija kwa Taifa na pia aanzishe miradi ya ndoto zake?

Hapa Kuna miradi yakitaifa na miradi ya maono binafsi ya JPM. Miradi yakitaifa ni mradi wa umeme wa rufiji, mradi wa reli, bomba la mafuta, ujenzi miundombinu ikiwemo umeme na kuboresha utoaji huduma.

Miradi ambayo haikuwa na sura ya kitaifa Ni ile iliyofanyika chako ikiwemo hifadhi,uwanja wa ndege, uwanja wa mpira, mahoteli na ofisi za umma nk

Katika miradi yote hii lazima kwa kauli moja Rais aseme Tanzania ina uwezo mdogo kiuchumi na kwamba nasimama na miradi ya kitaifa na endapo chenchi itabaki ntaangali chato. Asipofanya hivyo akasema anaendeleza kila alichoanzisha mzee JPM tutakwama.

Tumshauri Rais vyema
Atekeleze maono yake na kamwe asiendeleze yaliyopita, yalijaa ukienyeji.
 
YAANI NCHI IMEFIKIA HATUA YA KWENDA KWA NDOTO YA MTU MMOJA?
BUNGE BI LA NINI?
WIZARA NI ZA NINI?
INA MAANA MIRADI YA CHATO HAIPO KWENYE BAJETI ZA WIZARA?
 
Je, tunamshauri Rais mpya aendelee na miradi yote aliyoanzisha JPM au aendeleze ile miradi yenye tija kwa Taifa na pia aanzishe miradi ya ndoto zake?

Hapa Kuna miradi yakitaifa na miradi ya maono binafsi ya JPM. Miradi yakitaifa ni mradi wa umeme wa rufiji, mradi wa reli, bomba la mafuta, ujenzi miundombinu ikiwemo umeme na kuboresha utoaji huduma.

Miradi ambayo haikuwa na sura ya kitaifa Ni ile iliyofanyika chako ikiwemo hifadhi,uwanja wa ndege, uwanja wa mpira, mahoteli na ofisi za umma nk

Katika miradi yote hii lazima kwa kauli moja Rais aseme Tanzania ina uwezo mdogo kiuchumi na kwamba nasimama na miradi ya kitaifa na endapo chenchi itabaki ntaangali chato. Asipofanya hivyo akasema anaendeleza kila alichoanzisha mzee JPM tutakwama.

Tumshauri Rais vyema
Mh Samia Suluhu ndiye alikuwa mshauri mkuu wa JPM, hivyo atatekeleza miradi yote. Alishasema ataendelea pale JPM alipoishia. Anaifahamu hali ya uchumi wa Taifa.
 
Hiyo miradi haina faida yoyote kwa nchi awekeze kwenye kilimo cha kisasa ndicho kitakachowakwamua watanzania walio wengi kutoka kwenye umaskini.

Hii miradi aliyoianzisha Magufuli ilikuwa ni yake kwa ajili ya kujitafutia sifa huku ikiingiza nchi katika madeni makubwa ambayo baadaye itaifanya nchi ifilisike na hivyo kutokukopesheka.
 
Bora akajikita kwenye ilani ya uchaguzi ya chama chake na hayo maono yake! Kiufupi tu ni kwamba, hizo ndoto za Magufuli ni majanga/mateso kwa watu wengi.

Watumishi wa umma tutamkumbuka daima kwa kutudhulumu stahiki zetu kwa kisingizio cha kununua ndege na kujenga stiglers gorge.
 
Magufuli alikuwa anakurupuka kufanya kika kitu bika kufuata ushauri wa wataalamu.

Na as such kuna matumizi mabaya ya fedha kwa kufanya miradi bila FEASIBILITY studies, kitu ambacho ni UWENDAWAZIMU. Alishauriwa asikate miti kwa ajili ya umeme wa STIGLER Gorge hakusikia. SGR anajenga vipande vipande, kuna sababu gani ya kuanza kujenga Mwanza - Isaka wakati Dodoma- Nzega hakuna kitu.

Mawazo ya kijinga ya kujenga uwanja wa ndege kijijini kwako Chato Ni UPUNGUANI wakati unajuwa kuwa ukishakufa inabakia kuwa Kama Gbadolite ya Mobutu.

Samia anapaswa afanye kwa ilani ya chama chake na ruhusa ya Bunge lake. Magufuli alikuja kugundua kuwa hata kufika 2025 SGR haiwezi kukamilika ndiyo akaanza kufukuza wabunge wa upinzani ili mwaka huo abadili Katiba aendelee.

Mungu kamshtukia, kamnyofoa yeye kwanza ili Tanzania yetu irudi kwenye njia salama. Alikuwa anatuoeleka kwenye umaskini kama wa Zimbabwe
 
Kama kipo kwenye ilani yetu ya ccm ngumu kukitema kama hakipo tupa kule. Weka vyako.
 
Back
Top Bottom