Rais Samia Suluhu azindua mtambo wa kisasa taasisi ya moyo Jakaya Kikwete. Asema Kazi ilifanyika Awamu ya Tano

Rais Samia Suluhu azindua mtambo wa kisasa taasisi ya moyo Jakaya Kikwete. Asema Kazi ilifanyika Awamu ya Tano

kipara kipya

JF-Expert Member
Joined
May 2, 2016
Posts
18,833
Reaction score
23,276
Mambo yanaendelea huko tufuatilie kasi ni ile ile kazi iendelee.

========



Rais Samia Suluhu ameongoza shughuli za kuzindua Mitambo na kwa sasa zoezi linaloendelea salamu za watu mbali mbali. Alianza Professa Janabi ambae ametambulisha watu wote anaofanya nao kazi kila siku. Dkt. Janabi ametambulisha madaktari Bingwa wa Moyo nchini na kuelezea 'succession plan' kwenye taasisi yao endapo yeye ataondoka ama baadhi ya watu katika taasisi hiyo.

Baada ya Dkt. Janabi alifata Mkuu wa Mkoa wa Dar, Amos Makalla ambae ameongea kwa mara ya kwanza leo mbele ya Rais tangu kuteuliwa. Amos Makalla amemshukuru Rais Samia kumteua kuwa mkuu wa Mkoa wa Dar na kusema kwake ni nyumbani sehemu aliyozaliwa na kukulia. Makalla ameahidi kuendelea kukomesha Ujambazi Dar es Salaam.

Kisha akafata mkuu wa bodi ya Taasisi ya Jakaya Kikwete na kuelezea ndoto zake za kutibu magonjwa ya Moyo nchini na wengine kumkejeli mpaka ndoto zake kuwa kweli. Mwenyekiti ameelezea ndoto yake ya kuweza kuwa na watu mikoani watakaokuwa na uwezo wa kutibu magonjwa ya Moyo.

Anaongea Rais Samia na anasema kazi anayozindua leo ilifanyika awamu ya Tano na kumpongeza Hayati Rais Magufuli. Rais Samia amesema ameona uchawi unaofanyika ndani ya taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete. Amesema Tanzania inajisifu kwa kupunguza vifo vya watoto.

Rais Samia amesema eneo la Jakaya Kikwete limesaidia kupunguza vifo vya watoto. Amesema wagonjwa 5959 wamepata matibabu na watu 11 pekee wamefariki baada ya Upasuaji ikiwa ni asilimia 0.2 pekee. Ameongeza kusema mitambo pekee haitoshi kwani inaongozwa na watu na kuitumia ipasavyo.

Anasema ukisikia kusimamishwa moyo unakufa kabla haujasimamishwa lakini ndani ya taasisi ya Jakaya Kikwete unasimamishwa mpaka masaa sita.

Ameeleza kuzibeba changamoto zao na wanaenda kuzifanyia kazi.

Rais Samia amesema mcheza kwao hutuzwa na serikali itaangalia Maslahi yao.

Rais Samia Suluhu amewaahidi Bilioni mbili kutoka Serikalini kama walivyoomba kwa ajili ya kujenga jengo jipya, wao Taasisi ya moyo watatoa bilioni 2 kukamilisha bilioni 4 kwa ajili ya ujenzi huo


Samia Suluhu Hassan.jpg
 
Pia ni nafasi yake ya kubuni miradi mipya kwa awamu yake( awamu ya sita ) asilale na kuamka akizindua miradi iliyokuwepo au iliyoanzishwa awamu ya Tano tu.
Mwinyi alizindua ya Nyerere, Mkapa akazindua ya Mwinyi, Kikwete akazindua ya Mkapa na marehemu Magufuli akazindua ya Kikwete hiyvo si ajabu Samia nae kufungua ya Magufuli wote wanatekeleza ilani moja ya chama cha mapinduzi kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania!
 
Mwinyi alizindua ya nyerere,mkapa akazindua ya mwinyi,kikwete akazindua ya mkapa na marehemu magufuli akazindua ya kikwete hiyvo si ajabu Samia nae kufungua ya magufuli wote wanatekeleza ilani moja ya chama cha mapinduzi kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzan

Mwinyi alizindua ya nyerere,mkapa akazindua ya mwinyi,kikwete akazindua ya mkapa na marehemu magufuli akazindua ya kikwete hiyvo si ajabu Samia nae kufungua ya magufuli wote wanatekeleza ilani moja ya chama cha mapinduzi kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania!
Ufaransa yaipa Tanzania mkopo wa Tsh. Bilioni 361.7 kuzalisha umeme wa jua.....mradi wake huo.
 
Back
Top Bottom