Rais Samia Suluhu azindua mtambo wa kisasa taasisi ya moyo Jakaya Kikwete. Asema Kazi ilifanyika Awamu ya Tano

Huu mtambo ilitosha tu kufanya ziara na kusepa zake sio haya mambo ya sherehe sijui kuzindua aaahhh
Kwa taarifa tu uzinduzi una umuhimu wake. Mfano kama umefatilia kauli,maelezo na hotuba za Mhe. Rais, Prof. Janabi.Prof. Mahalu, Dr. Gwajima na wataalamu wengine wa JKCI utakuwa umeelewa umuhimu wa tukio hili. Nimeguswa sana na maelezo mafupi ya mwenyekiti wa bodi ya JKCI Prof. Mahalu juu ya ndoto zake. Nawapongeza JKCI kwa kazi, maelezo na hotuba nzuri.
 
Haya
 
Kwanini Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan kutamka vizuri neno Kuongeza linamshinda na badala yake hutamka ( husema ) Kuengeza mara kwa mara tu?
 
Kazi ilifanyika awamu ya tano ndio ambacho watanzania wanataka kusikia? Hizo ni kodi zao tusipende kuwapa sifa watu binafsi. Nairobi hospitali za uchochoroni zina mitambo kama hiyo.

CCM ilituchelewesha sana.
 
Kwanini Rais Mheshimiwa Mama Samia Suluhu Hassan kutamka vizuri neno Kuongeza linamshinda na badala yake hutamka ( husema ) Kuengeza mara kwa mara tu?
Lafudh ya kizanzibar imemuathir mkuu wazenj wengi Hilo neno kulitamka n mtihani

"Ushanfaham"
 
Pia ni nafasi yake ya kubuni miradi mipya kwa awamu yake( awamu ya sita ) asilale na kuamka akizindua miradi iliyokuwepo au iliyoanzishwa awamu ya Tano tu.

Kuhusu kubuni miradi mingine mipya usipate taabu maana mi15 tena ya kuwa rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania πŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈπŸƒβ€β™€οΈ
πŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒπŸ˜ƒ
 
Mama Samia atoe ajira 40,000 alizoahidi mei mosi. Vijana huku wana hali mbaya sana. Tumesomesha kwa gharama kubwa halafu wadogo zetu wanaendesha bodaboda!!!!
 
Ah! Mtambo bilion 4 nao tunazindua eti... B4 kwa serikali ni sio kitu cha kukiletea mbwembwe tena rais bora hata angezindua waziri au pm
Usiwe mtumwa wa fedha au financial mercenary yaani kila jambo unalithaminisha kifedha tu. Thaminisha na mambo mengine kama kuokoa maisha, kurahisisha matibabu, kuongeza ajira, ujuzi na maarifa, kupunguza umaskini, utegemezi wa nje, kuitangaza nchi n.k.
 
Mama Samia atoe ajira 40,000 alizoahidi mei mosi. Vijana huku wana hali mbaya sana. Tumesomesha kwa gharama kubwa halafu wadogo zetu wanaendesha bodaboda!!!!
Hizi zilizosemwa hapa ni mpya au zile ambazo muda wake wa maombi ushapita?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…