Rais Samia Suluhu Hassan afanya uteuzi wake wa kwanza Ikulu. Gerson Msigwa atolewa Ikulu, Dotto James ahamishwa. TPA, TCRA na TRA zapata wakuu wapya

Na mtazamo wako uko sahihi kabisa.ni mambo ya kipumbavu kabisa tunayokazana nayo
 
Aise naona mama anafanya kweli

Ova
Kila Rais anapoingia madarakani, anakuwa na ajenda zake za kipaumbele, na ili aweze kuzitekeleza ni lazima awapate watu ambao yeye binafsi anaamini wataenenda naye kikamilifu katika kuzitekeleza.
 
Watu wa clearing wanalia sana

Ova
Walibanwa Sana saizi zimebaki kampuni chache. Ukipita mitaa ya Clock Tower,Samora na Stesheni kumepoa huoni tena raia wakiwa wamevaa shati za light blue mikononi wameshika bahasha za documents wakikimbizana.
 
Wakati mwingine akili ndo inatakiwa kuongoza kichwa chako hv kuna jamii gani kwa Tanzania kwa sasa ambayo haina wasomi ?
Wapo ila sio wabobezi..tukubali tukatae kuna jamii ziko na wasomi wengi kuliko zingine hili huwezi pinga..mfano wahaya na wazaramo..lazima utapata wahaya wengi ni wasomi wabobezi wa ngazi za juu ukilinganisha na wazaramo..si leti ukabila ama udini ila ki uhalisia iko hivyo ukubali ukatae..chamsingi jamii zetu sasa zijikite kujipatia elimu ya kutosha.

#MaendeleoHayanaChama

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ndugu yangu kwa Dunia ya sasa ni ngumu sana watu wameamka wanapeleka watu shule unaposema wabobevu unamaanisha nini? Nitajie wote waliochaguliwa kuanzia makatibu wakuu,wakurugenzi nitajie mmoja tu ambae utasema ni mbobevu ambapo huwezi kumpata katika jamii nyingine.
 
Japo mimi niko kwenye lile kundi linalosisitiza Samia asipangiwe, aachwe afanye vile anaona inafaa, lakini kuhusu huu uteuzi usiozingatia kabisa gender balance, honesty, I don't believe huyu ni Samia huyu niliye zungumza hapa!.

Jee inawezekana Tanzania ni hatuna wanawake wa kutosheleza gender balance?, au wapo wamesahaulika?.
P
 
Mara nyingi nimekuwa nikijiuliza swali moja tu, hao viongozi wetu wanao teuliwa ktk nafasi mbali mbali kama vile Mawaziri, Manaibu, wakurugenzi n.k wote wanaonekana wana faaa na wana ujuzi wa kutosha kufanya kazi kwa mafanikio makubwa, lkn mbele ya safari unaanza kusikia mtu huyu huyu anaanza kutuhumiwa kwa kashfa za UBADHIRIFU wa mali za umma na RUSHWA.
Swali;
1. Je? nini haswa kinacho wafanya baadhi ya wateuliwa kubadilika mbele ya safari na kupoteza Uaminifu na kuwa wabadhirifu wa mali za Umma?
 
Huyu daktari nina wasiwasi nae sana, kama nakosea Mungu anisamehe. Kwanza najiuliza alikuwa nani kabla hajawa daktari wa Rais?
Alikuwa Dr Bugando, akahamia Chato kumhudumia Rais ndipo akapanda kuwa Katibu Mkuu Afya kipindi Corona imeitandika nchi kwa mara ya kwanza akimtoa Mama aliyekuwepo na naibu Dr Ndugulile wakaondolewa, alibaki na Ummy
yeye alisema Corona ni mafua makali yataondoka kwa nyungu na ndiye aliyeratibu na kudai hata papai lina Corona
Maana yake angekuwa mkweli na kukemea km wenzake Rais wetu angevaa barakoa na kujikinga, huenda mzigo wote walimuacha peke yake ili athibitishe mpendwa hatunaye tena kwa ugonjwa
 
Exemplary correct. Tena hiyo list ina watu wabovu wengi mno.
 
Msemaji Mkuu wa Serikali ni mtu mkubwa sana kuliko mnavyofikiria vijana.
Hiyo post ni imminent sana kwa exposure ya nchi na hata usalama wake. Msiichukulie poa kabisa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…