Ngosha Mashine
JF-Expert Member
- Sep 21, 2017
- 665
- 1,360
Kwako Mheshimiwa. Samia Suluhu Hassan
Pole na majukumu mama, mtangulizi wako ambaye pia ulikuwa msaidizi wake aliua kabisa matumaini ya wakulima kutajirika
Mama yaani miaka yake(yenu ukiwa msaidizi wake) bei za mazao zimekuwa chini sana wakulima wanaumia wanaonufaika ni wanunuzi(walaji)
Hebu angalia mfano mkulima wa mpunga aliepo Kahama, anakodi eneo la hekali moja kwa Tsh 150,000/- analima kwa Tsh 50,000/- anavuluga kwa Tsh 40,000/- anapanda kwa Tsh 40,000/- anaweka mbolea mfuko mmoja Tsh 70,000/- mpaka hapo anakuwa ametumia Tsh 350,000/-
Ukifika wakati wa palizi anatumia Tsh 40,000/- hapo anasubiri mpunga uchanue aanze kufukuza ndege, unafika wakati wa kuvuna wavunaji kukata anatumia Tsh 40,000/- wapigaji pia Tsh 40,000/- anapata gunia 20 za huo mpunga kama mavuno, ananunua mifuko 20 kwa @ Tsh 700/- mmoja = Tsh 14,000/- ausombe huo mpunga kutoka majarubani kuuleta eneo la kueleweka ili uende stoo kwa Tsh 1000/- kila gunia inakuwa Tsh 20,000/- Hapa inakuwa Tsh 114,000/- ukijumlisha na ile Tsh 350,000/- inakuwa Tsh 464,000/-
Hapa ni nje ya gharama za usafiri, chakula nk inafika wakati wa kuuza sokon anakutana na bei ya Tsh 35,000/- kwa gunia, magunia yake 20 anakuwa ametengeneza Tsh 700,000/- kwa muda wa zaidi ya miezi mitano.
Nadhani mheshiwiwa unaona njinsi anavyobaki na faida kidogo kama Tsh 236,000/ kwa muda wote huo yaani hela inayozidiwa na posho ya siku ya Mbunge.
Mama rudisha masoko ya nje bei ipae vijana wajiajiri kupitia kilimo kwa sababu watakuwa na uhakika wa kupata faida nzuri, mda huu vijana wengi wapo mijini wanaamini bora huko wafanye biashara ndogo ndogo kuliko kulima.
Utasuruhisha sana ugomvi wa bajaji na daradara mijini maana ndio kimbilio la sasa la vijana wako, polisi watapiga dolia sana kutafuta vibaka wanaoshindwa kuishi baada ya kukimbia mashambani.
Lakini Mama sekta hii ya kilimo ndio uti wa mgongo wa Taifa letu, wekeza huku Mama wewe usiishie kuongea tu bila kutatua matatizo na hapa Mama nikuambie tatizo kubwa ni bei bei ikipaa utaona vijana watavyowekeza huku.
Mama nisikuchoshe, ahsante natumai utayapokea haya nakusalimu kwa jina la Jamhuri ya muungano wa Tanzania.