Rais Samia Suluhu kumshukuru kwa ishara mhudumu wa Air Tanzania ni ishara ya Utumishi unaoheshimu wadogo na wakubwa

Rais Samia Suluhu kumshukuru kwa ishara mhudumu wa Air Tanzania ni ishara ya Utumishi unaoheshimu wadogo na wakubwa

Beatrice Kamugisha

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2019
Posts
762
Reaction score
6,984
Wakati Mhe. Rais anaingia jijini Dar akitokea Dodoma ameonekana akitoa shukrani kwa muhudumu wa ndege Jambo ambalo viongozi wengi awafanyi kwa watumishi wa chini yao.

Viongozi wengi wanapopata madaraka wamekuwa watu wa dharau na kufoka kwa walio chini yao. Wengi wamekuwa watu wakuona mapungufu kwa wadogo na si mazuri.

Nikupongeze Mhe. Rais kwa ulichokifanya, najua ukujipanga kufanya hivyo ila umefanya kwa sababu ndivyo ulivyolelewa na kukuzwa. Ila baada yakufanya hivyo sisi wa chini yako na wananchi tumeitafsiri hii Kama ishara yakurudisha nidhamu na heshima ndani ya Utumishi na jamii kwa mkubwa kumheshimu mdogo kadhalika kwa mdogo kumheshimu mkubwa.

Umemtia moyo sana huyo muhudumu wa ndege lakini pia umewatia moyo wengi waliokuwa na hofu dhidi ya watu wenye madaraka.

Niwatake viongozi wengine mjifunze kuheshimu walinzi, wapishi, wafanyakazi wa ndani, wahudumu, wasaidizi na kila mtu unayeinteract naye katika maisha binafsi na maisha ya kazi. Tuache kujimwambafai tukiamini titaogopeka.

Respect my president.
 
Wewe mama wa Kihaya una macho yanayoona mbali sana, imenibidi nitafte hii clip kuona unalolisema. True anaonekana akishukuru, Kwanza kitendo Cha kumwona huyu muhudumu wakati tumezoea viongozi wengi uelekeza macho kwa wenyeji wao ni ishara ya makuzi. Huu unaitwa uongozi unaoacha halama bila kutumia maneno. Hii video naidownload kiongozi akifoka namtag😂😂😂😂😂kumkumbusha zama za kufokafoka zimepita sisi sote ni binadamu tuna Hali yakuheshimiwa na tutaadhibiwa baada yakuthibitika tuna hatia
 
Kweli kbs tusiwe kama yule mwenyekiti wa chama fulan ambae mwaka 2015 alipuuza ushauri na matakwa ya wanachama wake kwa kuamua kumpitisha yule fisadi papa agombee uraisi kupitia chama chake bila kufuata utaratibu mzuri na ushauri wa waona mbali, wakiwemo wasomi wakubwa wa chama hicho. Sipati picha kama mwenyekiti huyu angekuwa au akiwa raisi anaweza kusikiliza ushaur wa mtu yoyote au kujishusha kama alivyofanya raisi unaemzungumzia hapa. Japo wanachama walimtaka yule dr Slaa lkn yeye kwa kuangalia masilahi ya tumbo lake akaamua iwe ilivyokuwa. Alikataa kujishusha kwa kufuata ushaur wa wanachama wake walio wengi na alitumia uenyekiti wake na kiburi kuamua aliyoyataka yeye
 
Yaani Rais hata akikohoa kwa sasa utaanzishwa Uzi. Ni mwendo wa kusifu kinafikii tu.
 
Mbona kawaida marais wengi wanafanya hivyo Ila nawakubali Sana Trump Kuna siku alikuwa anaboard airforce one ( helcopter) Kuna mhudumu Askari alikuwa amekakamaa kwa saluti mlangoni upepo ulikuwa mkali kofia ya yule Askari ikapeperushwa na upepo ikaanguka , Trump aliinama akachukua ile kofia akamvalisha yule Askari halafu naye Trump akampigia saluti yule Askari.
Trump alikuwa very gentleman kwa watu wa chini
 
Wakati Mhe. Rais anaingia jijini Dar akitokea Dodoma ameonekana akitoa shukrani kwa muhudumu wa ndege Jambo ambalo viongozi wengi awafanyi kwa watumishi wa chini yao.

Viongozi wengi wanapopata madaraka wamekuwa watu wa dharau na kufoka kwa walio chini yao. Wengi wamekuwa watu wakuona mapungufu kwa wadogo na si mazuri.

Nikupongeze Mhe. Rais kwa ulichokifanya, najua ukujipanga kufanya hivyo ila umefanya kwa sababu ndivyo ulivyolelewa na kukuzwa. Ila baada yakufanya hivyo sisi wa chini yako na wananchi tumeitafsiri hii Kama ishara yakurudisha nidhamu na heshima ndani ya Utumishi na jamii kwa mkubwa kumheshimu mdogo kadhalika kwa mdogo kumheshimu mkubwa.

Umemtia moyo sana huyo muhudumu wa ndege lakini pia umewatia moyo wengi waliokuwa na hofu dhidi ya watu wenye madaraka.

Niwatake viongozi wengine mjifunze kuheshimu walinzi,wapishi,wafanyakazi wa ndani,wahudumu,wasaidizi na kila mtu unayeinteract naye katika maisha binafsi na maisha ya kazi. Tuache kujimwambafai tukiamini titaogopeka.

Respect my president.
Hata picha tu kuonesha tendo hilo umeshindwa kutupatia?
 
No
Mwendazake alikuwa anafokafoka kuanzia tarehe moja mpaka tarehe moja, January mpaka December hata akienda kusali ye ni kufoka tu na vitisho
No Wonder alipata matatizo ya moyo, muda wote ana hasira tu why?
 
Back
Top Bottom