Natoa ushauri kwa Serikali, Itumie zoezi hili la sensa kama fursa ya kurekebisha kero zote zinanowakumba watu wa mipakani kuhusu uraia. Naamini kuwa lengo la Serikali ni kujua idadi ya watanzania, kwa maana hiyo kila atakayehesabiwa atakuwa ni mtanzania bila kujali anaishi mpakani au katikati ya eneo la JMT.
Ili kuepuka usumbufu wanaoupata watu wanaoishi katika mikoa ya mipakani na hasa kurahisisha zoezi la kumtambua mtanzania kwa mamlaka husika, baada ya mtu kuhesabiwa Serikali itoe cheti au hati inayothibitisha kuwa mwananchi amehesabiwa kama mtanzania.
Kama baada ya miaka ya utoaji wa elimu katika ngazi zote za msingi upili au chuo huhitimishwa kwa kutoa cheti, sioni ugumu wowote kwa Serikali kutoa cheti cha sensa inayofanyika kila baada ya miaka kumi na zaidi.