Rais Samia Suluhu ni kiongozi na mlezi mahiri wa Taifa

Rais Samia Suluhu ni kiongozi na mlezi mahiri wa Taifa

Ngaliwe

Senior Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
164
Reaction score
374
Uwezo wa kiuongozi wa Rais Samia unazidi kujipambanua dhahiri kadiri siku zinavyosonga mbele. Na sasa amegusa jambo muhimu sana na la msingi zaidi katika ujenzi wa Taifa lolote lile kwa ajili ya maendeleo endelevu.

Katika mazungumzo yake na wazee wa Dar es Salaam hivi karibuni, pamoja na mambo mengine aligusia jambo muhimu sana kwa mustakabali mwema wa Taifa letu. Umuhimu wa kutunza na kuheshimu wazee katika jamii zetu.

Hata kama suala hili halikuonekana kama ni hoja muhimu kwenye vyombo vyetu vya habari, kwa kuwa vimeathrika sana na masuala ya kisiasa, hilo halilipunguzii umuhimu wa suala hilo. Utamaduni na mila za kila jamii ndiyo msingi wake mkuu wa uendelevu wa jamii hiyo. Kama ni lazima jamii hiyo iendelee hapana budi isipokuwa kujenga na kuegemza maendeleo yake katika misingi hiyo muhimu ili yawe endelevu na yenye manufaa kwa wanajamii wengi wa jamii husika.

Na katika Tanzania tunajua kwa uhakika kuwa mwanzo kabisa wa jamii zetu hizi, hapakuwa na matatizo ya kijamii tuliyo nayo leo. Katika jamii za kifrika ilikuwa ngumu sana kukutana na omba omba, watu wasiokuwa na makazi (wanaolala kwenye vituo vya mabasi au viambaza vya maduka mijini), watoto wa mitaani na mengine. Hii haikutokea kwa bahati mbaya ilitokana na ubora wa misingi ya utamaduni na desturi njema zilizowekwa na wazee ili kumhakikishia kila mtu hifadhi ya jamii.

Hifadhi ya jamiii zetu iliwekwa vizuri kabisa katika mfumo wa familia ambapo familia ziliweza kubainisha matatizo yanayowakabili na kuweka utaratibu wa namna ya kuyatatua. Moja ya njia hizo ni zile za kulea ndugu au watoto wa wanafamilia wenye matatizo.

Mfano watoto yatima waliweza kutunzwa na kulelewa na ndugu wa baba au mama yao kwa hadhi na heshima kama tu watoto wa familia hiyo. Wengi wetu leo wanakumbuka jinsi familia zao vijijini zilivyokuwa na watu wengine na ambao walikuwa na kuwaheshima kama ama kaka au dada zao wa kuzaliwa nao, wajomba au shangazi zao kabisa lakini kumbe walitoka ukoo wa mbali, wazee walihakikisha wanamlea kila mtu katika familia kwa usawa ndiyo maana wengi walikuja kugundua kuwa kaka au dada waliyekuwa wanajua wamezaliwa naye tumbo moja, alikuwa mtoto wa mjomba au binamu yake, hiyo ndiyo ilikuwa thamani ya mila na desturi njema za Kiafrika.

Mfumo huu uliwahakikishia wana jamii wengi uhakika wa hifadhi ya jamii, hata walipokosa wazazi, watoto walikuwa na uhakika wa kuishi maisha ya utu na bora kwa viwango vya jamii husika, waliozeeka na ama hawakuwa na watoto au watoto wao wamewatangulia mbele za haki, walipozeeka na kukosa uwezo wa kujitegemea walikuwa na uhakika wa kuendelea kuishi maisha yenye utu, heshima na staha inayomstahili binadamu kwenye familia za ndugu zao. Hii iliihakikishia jamii kutokuwa na watoto wa mitaani, wazee omba omba na changamoto tunazoziona leo.

Tulipotoka njia pale tulipokumbatia utamaduni wa magharibu wa ubinafsi (individualism) na kuacha kujaliana na kuthaminina kama wanafamilia na kama watu wa jamii moja kupitia malezi kwenye familia pana (extended family).

Alichofanya Rais ni kutukumbusha kwamba msingi wa kweli wa maendeleo yetu lazima ujengwe juu ya jamii imara iliyoshikamana na inayoheshimu na kuthamini utu wa kila mtu. Ndiyo maana hatua na Rais Samia kutufunda kuhusu umuhimu wa kujenga jamii inayoheshimu misingi ya utu wa mtu ni muhimu sana.

Hii imedhihirisha tena, bila shaka uwezo wa Rais Samia wa namna anavyoweza kulipeleka Taifa letu mbali, kwa kuwa maono yake yanaitafsiri vyema na kuibua misingi muhimu sana ya kujenga jamii inayojitambua na kuheshimu utu wa watu.

Ukishakuwa na misingi imara namna hii iliyojikita vyema kwenye jamii ni rahisi na haraka mno mipango na juhudi za ujenzi wa taifa kwa maendeleo ya kiuchumi kuweza kutekelezwa na kuleta manufaa kwa jamii nzima.

Rais Mama Samia ametuonyesha njia ya kupita, turejee kwenye misingi yetu ya utu na ubinadamu, tujitazame upya, ili kwayo tujenge juu yake maendeleo yetu na kwa kufanya hivyo tutakuwa tunajenga juu ya msingi imara na uchumi wetu hauwezi kuteteleka. Inawezekana tutimize wajibu wetu.

Asante SAMIA
 
Kipindi chote cha Marais wetu, Tumekuwa tukiwasifu na kuwaponda, lakini licha ya hivyo, hakuna tulichokipata, Mimi nadhani, kuanzia sasa, ni vema tukawa ni watu wenye kiasi
 
Wewe ulionana na daktari lini? Nenda upime akili Yako because what you are writing here is crap. Siasa ni kula hela zetu. Juzi altuambia serikali haina hela kesho yake Anagawa majumba na magari. Ni huyu huyu alituambia Magufuli yuko ok kumbe kisha Kufa kwa mzena hospital.
 
Wewe ulionana na daktari lini? Nenda upime akili Yako because what you are writing here is crap. Siasa ni kula hela zetu. Juzi altuambia serikali haina hela kesho yake Anagawa majumba na magari. Ni huyu huyu alituambia Magufuli yuko ok kumbe kisha Kufa kwa mzena hospital.
Kumbuka kuwa shughuli ya uzinduzi wa kitabu ilikuwa ifanywe na Hayati Magufuli mwezi wa tatu. Kumbuka kuwa zawadi ya gari ilikuwa itolewe na Hayati pia.
 
Kumbuka kuwa shughuli ya uzinduzi wa kitabu ilikuwa ifanywe na Hayati Magufuli mwezi wa tatu. Kumbuka kuwa zawadi ya gari ilikuwa itolewe na Hayati pia.
Kumbuka kuwa shughuli ya uzinduzi wa kitabu ilikuwa ifanywe na Hayati Magufuli mwezi wa tatu. Kumbuka kuwa zawadi ya gari ilikuwa itolewe na Hayati pia.
Asante kwa majibu, naona Kama utakuwa RC hivi karibun. Vipi tulivyodanganywa Magufuli yupo tu, Hilo walionaje?
 
Ikulu ni mwendo wa barakoa. Corona ni noma kule India nchi inakaribia kuwa jangwa, miti yote inaisha kwa sababu ya kuchoma moto maiti zao.
 
Back
Top Bottom