Rais Samia Suluhu ni wakati kulihutubia Taifa kuweka mambo sawa

Rais Samia Suluhu ni wakati kulihutubia Taifa kuweka mambo sawa

PAZIA 3

JF-Expert Member
Joined
Jan 30, 2018
Posts
1,102
Reaction score
1,919
Rais Samia Suluhu huu si wakati wa kukaa kimya, hutubia taifa ili nchi na watu wake wapate mwanga mpya, kuna mambo mengi yanachanganya wananchi, mfano
  • Suala tozo
  • Chanjo
  • Democracy
  • Ugaidi
Kuna kipindi Rais JMK mstaafu na Dkt. John P Magufuli walizungumza na taifa pale ilipotokea kukawa na kelele nyingi.

Ukihutubia taifa, haijalishi utasema Nini ila utabadilisha upepo na kuleta hoja mpya kwa wananchi.

Isitumike nguvu kunyamazisha Uhuru wa maoni ya watanzania haijalishi ni ccm au upinzani

"Hoja haipigwi rungu" jmk
 
Ahutubie Taifa?

Mbona siku hizi wananchi ndio wanaohutubia kwa watawala.
 
Mambo yakiharibika zaidi hawa hawa CCM watamgeuka, kwa mfano sasa hivi tayari CCM imeshagawanyika kuhusu msimamo wa chanjo ya Covid-19, Mzimu wa Mwendazake umeanza kuwatesa taratibu.l
 
Gaidi Mbowe ndio amsumbue Rais kuhutubia taifa bila ya kuwa na ratiba hiyo?

Gaidi Mbowe yupo sehemu stahili, chawa wake mtulie, kama mna uchungu sana nendeni mkajiunge naye Ukonga.
 
Hakuna haja ya kumpa pressure.

yeye ni rais wa jamhuri sio wa wanaharakati
 
Maza kapoteza mwelekeo kabisa hata haeleweki anasimamia nini
 
Ataongea nini maushungi huyu?? Nchi inakwenda msobe msobe tu.
 
Rais Samia Suluhu huu si wakati wa kukaa kimya, hutubia taifa ili nchi na watu wake wapate mwanga mpya, kuna mambo mengi yanachanganya wananchi, mfano
  • Suala tozo
  • Chanjo
  • Democracy
  • Ugaidi
Kuna kipindi Rais JMK mstaafu na Dkt. John P Magufuli walizungumza na taifa pale ilipotokea kukawa na kelele nyingi.

Ukihutubia taifa, haijalishi utasema Nini ila utabadilisha upepo na kuleta hoja mpya kwa wananchi.

Isitumike nguvu kunyamazisha Uhuru wa maoni ya watanzania haijalishi ni ccm au upinzani

"Hoja haipigwi rungu" jmk
Umesahau madai ya KATIBA mpya.
 
Gaidi Mbowe ndio amsumbue Rais kuhutubia taifa bila ya kuwa na ratiba hiyo?

Gaidi Mbowe yupo sehemu stahili, chawa wake mtulie, kama mna uchungu sana nendeni mkajiunge naye Ukonga.
Chuki zitakupeleka pabaya sana.
Siasa hazina uadui huo unaujaza kichwani kwako
 
Gaidi Mbowe ndio amsumbue Rais kuhutubia taifa bila ya kuwa na ratiba hiyo?

Gaidi Mbowe yupo sehemu stahili, chawa wake mtulie, kama mna uchungu sana nendeni mkajiunge naye Ukonga.

Ww lazima utakuwa ni mzee, nakushauri ukachanje covid, usije ukapotea siasa za kizee zikaisha ccm.
 
Yeah! Ni wazo zuri kutoa muelekeo wake kwenye key issues.
Tozo
Sio lengo la serikali kuwaumiza wananchi lakini pia serikali ina wajibu wa kutoa ajira mpya na huduma za jamii. Nchi yetu imechoka kutembeza beseni kwa wahisani hivyo katika harakati za kujitegemea inabidi tujipige pige.
Hata hivyo kwa kuwa bajeti imeshapita, basi swala hili atalivalia njuga kwenye bajeti ijayo. Hata hivyo bado wanaangalia mianya iliyopo kisheria ya kumpunguzia makali mwananchi.
Awahimize wananchi kuendelea kutumia miamala ya simu kwa wingi ili kushiriki kuchangia tozo za kizalendo.

Katiba
Yeye pia ni mwana mabadiliko na pale panapotokea nafasi ya kuboresha kitu chochote kinachomhusu mwananchi, naye yuko mstari wa mbele kuunga mkono maboresho hayo.
Yeye pia aunge mkono maboresho ya katiba lakini asisitize kuwa maboresho hayo yanahitaji maandalizi hasa ya kifedha. Kwa wastani mchakato wa maboresho ya katiba mpya huweza kuligharimu taifa kiasi cha bilioni hamsini na fedha hizo kwa sasa hazikutengwa hivyo wampe muda aweze kuangalia uwezekano wa kupatikana fedha hiyo kwenye bajeti ya mwakani ili kuruhusu mchakato kuanza.
Sambamba na hilo awaagize polisi kuwapa dhamana wale wote waliokamatwa kwenye harakati za kuisaka katiba mpya bara barani huku akiwasisitiza wapinzani kutumia njia sahihi za kuisaka katiba iliyoboreshwa kwani katiba haipatikani bara barani.
 
Back
Top Bottom