Rais Samia Suluhu, stuka kabla hawajakuingiza mkenge

Msanii

Platinum Member
Joined
Jul 4, 2007
Posts
25,252
Reaction score
36,513
Mwaka 2015 niliandika maoni yangu hapa JamiiForums kumshauri Hayati JPM mara baada ya kuapishwa kushika nafasi ya Urais wa Tanzania.

Pamoja na kelele zinazopigwa hapa na pale lakini haiondoi ukweli kwamba wewe ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa majenzi ya Ulinzi na Usalama.

Umeanza kwa hatua nzuri sana tena zinazoacha bumbuwazi kwa wanaotarajia kuwa hautaweza kuitendea haki nafasi ulitoapishwa kuitumikia.

Nina machache mno ya kukushauri ingawa yanaweza kuonekana ya kijinga lakini unaweza kuyaangalia kwa jicho tofauti zaidi.

1. WASHAURI
Kuwa muangalifu na washauri wako gawa wa upande wa Siasa na Jamii. Hawa mara nyingi hupenda kujibadilisha na kuwa kingmakers.
Utaletewa majina ya uteuzi kwa nafasi mbalimbali, unaweza kuletewa na vertings zilizosheheni mbwembwe nyingi na produces facts lakini kumbe behind ya scene ni kukupelekea ufanye political blunders.

Wateule wa sasa ambao tayari wameshaonesha makandokando waweke pembeni weka watu wanaoendana na falsafa yako ya kuifungua nchi. Hawa waliopo unawajua na walitumika sana kuibana na kuifunga nchi ili kufanikisha malengo waliyopangiwa

2. UCHUMI
Vitambulisho vya Wajasiriamali ni incubator ya uchumi kwa wafanyabiashara wa chini waweze kupanda viwango. Ukiviboresha na kuviwekea details zinazompa uhalali anatekikata kuaminika kwenye microfinances irasaidia sana mzunguko wa uchumi kwa madaraja yote.

Iangalie Tanzania Chambers of Commerce kwa uangalifu sana. Ujiulize kwa nini uwiano wa uwekezaji wa Watanzania nje na wageni wanaowekeza kwetu hauko fair?

A. Fair Trade
Tanzania iliridhia mkataba wa Fair Trade kupitia WTO lakini hakuna juhudi za watendaji wako kuwaunganisha Watanzania kwenye soko hili kubwa ulimwenguni ambalo limeiinua sana Asia. Biadhaa nyingi za majirani zetu Wakenya ziinazopelekwa Fair Trade zinatoka hapa kwetu na wanaziwekea brand ya Kenya hivyo tunarudi kwenye story ya Tanzanite..

B. AGOA
Hii opportunity imetwaliwa na Wachina kupitia viwanda vya uwekezaji Ethiopia, Kenya na Zambia. Nafasi ingalipo na tunaweza kuliingia kwa kasi kubwa

C. REGIONAL TRADE
Hapa uangalie korido za SADC, EAC, EPA na mengineyo. Tunapofungua fursa kwa wawekezaji kutoka nje, je uwiano wa sisi kuwekeza huko kwao upoje? Je vigezo ni parallel au competetive?

D. TRADE INTEL
Hatuwezi kama Tanzania kufika mbele bila kuwa na ukusanyani na uchakataji wa taarifa mbalimbali zinazoweza kusaidia watu wetu kuwekeza maeneo ya nje yenye fursa.

AEGIS ni shirika binafsi lakini lina mkono wa serikali ya Uingereza ambalo kazi yao kubwa ni kuangalia, kulinda na kutafiti kwa maslahi ya wawekezaji wa Uingereza na baadhi ya sehemu ya Ulaya.

CIA inafanya ujasusi wenye maslahi ya kiuchumi kwa nchi ya Marekani.

Sisi siyo kisiwa,ni muhimu tuwe na kurugenzi au taasisi inayojitegemea inatofanya ujasusi wenye maslahi ya Tanzania kibiashara

3. ULINZI NA USALAMA
Wewe na mtangulizi wako mliiweka nchi yetu salama kabisa. Lakini haiondoi ukweli kwamba bado zipo chokochoko hususani jirani na mpaka wa Msumbiji, mpaka wa magharibi na kaskazini.

Ni vizuri ukaiangalia TAMISEMI hasa nafasi za viongozi wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa wapewe uwezo zaidi kwenye eneo hilo kusaidia kuiweka salama chini yetu.

5. SIASA
Mheshimiwa Rais, ruhusu vyama vya siasa vifanye shughuli zao. Tekeleza ahadi yako ya serikali mseto kusaidia kuiponya nchi.

Kuwa muangalifu sana na washauri wa Siasa.

IMG-20210507-WA0088.jpg
 
Katiba mpya ni jambo ambalo mchakato wake unapaswa kuanzishwa upya kabisaa.

Sijawahi kuwa na imani na Jaji Warioba. Katiba waliyoipendekeza inaelekeza kuvunja Muungano na kuongeza gharama za kuendesha Serikali.

Sera ya majimbo ni nzuri endapo itaboreshwa iwe tofauti na CHADEMA walivyotaka
 
VITAMBULISHO VYA TAIFA VITOLEWE KWA KABLA YA KUFUNGUA MILANGO NA MADIRISHS YA NCHI.
''NIDA" WATAMBUE KUWA RAIS AKIFUNGUA NCHI,TUNAENDA KUATHIRIKA NA KUSUA SUA KWAO KUTOA VITAMBULISHO KWA WANANCHI WA TANZANIA.
 
Huwa sielewi hayo majamaa hapo NIDA huwa yanafanya nini...alafu mijitu inalipwa.Shame kabisa!!!

Mbona vya kura huwa vinatoka within 1day?

Aaaarh
 
Huyo aliyekaa naye kwenye picha ndiye atakayemwingiza mkenge. Biashara zake zisizolipa kodi na biashara ya sembe kufanywa na mwana wa mfalme ndiyo zake huyo. Mama awe makini naye sana.
 
Katiba mpya ni jambo ambalo mchakato wake unapaswa kuanzishwa upya kabisaa.

Sijawahi kuwa na imani na Jaji Warioba. Katiba waliyoipendekeza inaelekeza kuvunja Muungano na kuongeza gharama za kuendesha Serikali.

Sera ya majimbo ni nzuri endapo itaboreshwa iwe tofauti na CHADEMA walivyotaka
Unaishia kusema ya Chadema iboreshwe weka maoni yako tusome

Sent from my Nokia 8.1 using JamiiForums mobile app
 
Hiyo point namba mbili naona linafanana na wazo langu nililowahi toa hapo awali. ; Nilifafanua zaidi;

Mwaka 2015 niliandika maoni yangu hapa JamiiForums kumshauri Hayati JPM mara baada ya kuapishwa kushika nafasi ya Urais wa Tanzania.

Pamoja na kelele zinazopigwa hapa na pale lakini haiondoi ukweli kwamba wewe ndiye Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye pia ni Amiri Jeshi Mkuu wa majenzi ya Ulinzi na Usalama.

Umeanza kwa hatua nzuri sana tena zinazoacha bumbuwazi kwa wanaotarajia kuwa hautaweza kuitendea haki nafasi ulitoapishwa kuitumikia.

Nina machache mno ya kukushauri ingawa yanaweza kuonekana ya kijinga lakini unaweza kuyaangalia kwa jicho tofauti zaidi.

1. WASHAURI
Kuwa muangalifu na washauri wako gawa wa upande wa Siasa na Jamii. Hawa mara nyingi hupenda kujibadilisha na kuwa kingmakers.
Utaletewa majina ya uteuzi kwa nafasi mbalimbali, unaweza kuletewa na vertings zilizosheheni mbwembwe nyingi na produces facts lakini kumbe behind ya scene ni kukupelekea ufanye political blunders.

Wateule wa sasa ambao tayari wameshaonesha makandokando waweke pembeni weka watu wanaoendana na falsafa yako ya kuifungua nchi. Hawa waliopo unawajua na walitumika sana kuibana na kuifunga nchi ili kufanikisha malengo waliyopangiwa

2. UCHUMI
Vitambulisho vya Wajasiriamali ni incubator ya uchumi kwa wafanyabiashara wa chini waweze kupanda viwango. Ukiviboresha na kuviwekea details zinazompa uhalali anatekikata kuaminika kwenye microfinances irasaidia sana mzunguko wa uchumi kwa madaraja yote.

Iangalie Tanzania Chambers of Commerce kwa uangalifu sana. Ujiulize kwa nini uwiano wa uwekezaji wa Watanzania nje na wageni wanaowekeza kwetu hauko fair?

A. Fair Trade
Tanzania iliridhia mkataba wa Fair Trade kupitia WTO lakini hakuna juhudi za watendaji wako kuwaunganisha Watanzania kwenye soko hili kubwa ulimwenguni ambalo limeiinua sana Asia. Biadhaa nyingi za majirani zetu Wakenya ziinazopelekwa Fair Trade zinatoka hapa kwetu na wanaziwekea brand ya Kenya hivyo tunarudi kwenye story ya Tanzanite..

B. AGOA
Hii opportunity imetwaliwa na Wachina kupitia viwanda vya uwekezaji Ethiopia, Kenya na Zambia. Nafasi ingalipo na tunaweza kuliingia kwa kasi kubwa

C. REGIONAL TRADE
Hapa uangalie korido za SADC, EAC, EPA na mengineyo. Tunapofungua fursa kwa wawekezaji kutoka nje, je uwiano wa sisi kuwekeza huko kwao upoje? Je vigezo ni parallel au competetive?

D. TRADE INTEL
Hatuwezi kama Tanzania kufika mbele bila kuwa na ukusanyani na uchakataji wa taarifa mbalimbali zinazoweza kusaidia watu wetu kuwekeza maeneo ya nje yenye fursa.

AEGIS ni shirika binafsi lakini lina mkono wa serikali ya Uingereza ambalo kazi yao kubwa ni kuangalia, kulinda na kutafiti kwa maslahi ya wawekezaji wa Uingereza na baadhi ya sehemu ya Ulaya.

CIA inafanya ujasusi wenye maslahi ya kiuchumi kwa nchi ya Marekani.

Sisi siyo kisiwa,ni muhimu tuwe na kurugenzi au taasisi inayojitegemea inatofanya ujasusi wenye maslahi ya Tanzania kibiashara

3. ULINZI NA USALAMA
Wewe na mtangulizi wako mliiweka nchi yetu salama kabisa. Lakini haiondoi ukweli kwamba bado zipo chokochoko hususani jirani na mpaka wa Msumbiji, mpaka wa magharibi na kaskazini.

Ni vizuri ukaiangalia TAMISEMI hasa nafasi za viongozi wa Vijiji, Vitongoji na Mitaa wapewe uwezo zaidi kwenye eneo hilo kusaidia kuiweka salama chini yetu.

5. SIASA
Mheshimiwa Rais, ruhusu vyama vya siasa vifanye shughuli zao. Tekeleza ahadi yako ya serikali mseto kusaidia kuiponya nchi.

Kuwa muangalifu sana na washauri wa Siasa.

well
 
Hiyo point namba mbili naona linafanana na wazo langu nililowahi toa hapo awali. ; Nilifafanua zaidi;

Uliwaza sahihi kabisa.

Unajua kwa kipindi kirefu sana Serikali inapambana kuwapatia mitaji wananchi wa hali ya chini kupitia program mbalimbali kama vile 10% ya mapato ya Halmashauri lakini kumekuwa na negligence kubwa kwa watendaji kuhakikisha mitaji inakua.

Hivyo ubunifu wa vitambulisho unawahakikishia wajasiriamali utulivu wa kibiashara jambo ambalo linafaa sana kwa ukuaji wa uchumi.

Hawa watu wadogo ndiyo watakaotupeleka uchumi wa kati nafasi ya juu na hatimaye kutoka hapo na kufikia waliopo mabeberu.

Wazo la BRELA ni zuri sana lakini waweke dirisha la Wajasiriamali pale pia
 
Tutofautishe awamu.

Hii ni Awamu ya Sita.

Rais Samia akiungwa mkono anaweza kutupeleka mbali zaidi ya hapa
 
Back
Top Bottom