Rais Samia Suluhu umeanza kuwa Dikteta mapema kuliko hayati John Pombe Magufuli

Rais Samia Suluhu umeanza kuwa Dikteta mapema kuliko hayati John Pombe Magufuli

seedfarm

JF-Expert Member
Joined
Feb 9, 2020
Posts
260
Reaction score
2,655
Kauli ya Rais Samia kuminya uhuru wa Raia na vyama vyao vya siasa kwa kutozingatia katiba na sheria ameingia kwenye rekodi mpya kama Rais Mwanamke wa kwanza Africa kuwa Dikteta.

Siku ya 101 madarakani, Rais Samia Suluhu tayari ameanza kulewa sifa na mapambio. Ameamua kuendelea kuminya uhuru wa vyama vya siasa kufanya mihadhara kwa kutumia utashi wake na siyo katiba iliyomfanya Yeye awe Rais bila kupigwa kura za wananchi.

Hakuna uchumi bila haki na uhuru wa watu, Tangu tupate uhuru kwa miaka zaidi ya ishirini na nne ya chama kimoja hakuna Uchumi wowote uliosimama, Uchumi ulianza kusimama wakati wa vyama vingi vya kisiasa na huu ni wakati wa Hayati Ben Mkapa, Hayati Ben Mkapa alisimamia uhuru na kujenga mfumo wa kitaasisi.

Mama Samia ameanza kuonyesha sura yake halisi ya udikiteta mapema sana, Atambue na akumbuke hakuna aliyempigia kura kwenye sanduku kama Rais wa nchi bali amepata Urais kwa kufuata katiba ya nchi, Wananchi wa Tanzania ni waelewa ndio maana Mama alipoapishwa kwa kufuata katiba hakuna aliyelalamika kwenye mitandao ya kijamii, Kuanza kuvunja katiba siku ya 101 kisa umesifiwa sana Jiandae kisaikolojia kwa watu kukusema kimataifa kama mtangulizi wako na kitakachofuatwa ni wewe kuhojiwa maswali Magumu na vyombo vya kimataifa ukajikuta unadhalilika na kutafuta mchawi nani.

Chuki ambayo umejenga kwa kauli yako ya kusema hakuna vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara umeitoa kwa kutumia sheria na katiba ipi? Wewe uliapishwa kwa kufuata katiba kwanini umeanza kuharibu na kupindisha katiba ya nchi?

Kauli yako ya kuminya uhuru wa siasa imekuharibia kila kitu na sasa mjadala umeanza kuwa mkali zaidi, Jiandae Kwa watu kukusema hovyo na kukudhalilisha zaidi ya mtangulizi wako.

Kila kauli ina madhara yake, Kauli yako ya kuwa unajenga Uchumi, Hayati Magufuli alisema analeta Maendeleo. Leo hakuna anayemkumbuka Magufuli na habari zake za Maendeleo bali anakumbukwa kwa kuminya na kukandamiza haki za Raia.

Serikali iwape watu uhuru wao, Kuna tetesi zilizagaa kuwa hata wewe watu walitaka usipewe Urais kwani waliona hutaweza lakini kuna kundi likasimamia katiba na ukaapishwa kuwa Rais, Kwanini wewe unavunja katiba?

---
UPDATE tarehe 02/07/2021
Mkutano wa wanawake wa Chadema (Bawacha) uliokuwa unafanyika kwenye ukumbi mikocheni umevamiwa na polisi kwa amri toka juu, Wamefukuzwa ndani ya dakika 30

Serikali ya Samia Suluhu ni ya kidikiteta kuliko ya Magufuli, Hawajaangalia gharama za ukumbi, Polisi kwa amri toka juu wameuvuruga mkutano


Updates 17/07/2021

Sasa ni marufuku kujadili mambo ya tozo za miamala ya simu iliyokuwa ya kinyonyaji, Mama amezuia mjadala wa katiba mpya, Ukitaka kujadili katiba mikusanyiko inavamiwa na polisi kwa amri toka kwa Rais Samia

Update 21/07/2021
Mbowe na wenzake wavamiwa hotelini kwa amri toka juu, Hawajulikani walipo

Ni amri toka juu, Wakiwa wa najiandaa kujadili katiba mpya


UPDATE 22/07/2021

Mbowe abambikiwa kesi ya ugaidi na Mamlaka
 
Ameanza kupandisha mabega. Spana ziendelee tu hakuna jinsi nyingine
Nilimkubali sana, ila kwa kauli hii na mimi naunga mkono. Maana hata Mtangulizi wake alianza hivihivi kwa kujifanya anaupiga mwingi kwa kuvuta hisia za wapinzani na wasio wanasiasa baadaye akawageukia ghafla. Hata huyu naona ndiyo anapokwenda
 
Hiyo Katiba iangaliwe upya, Mikutano ya kisiasa ISIWEPO mpaka muda wa Uchaguzi utakapofika.

Nchi zenye Demokrasia tangu miaka 200 iliyopita wanafanya siasa za hadharani inapokaribia Uchaguzi husika.

Sisi Tanzania tunataka miaka mitano mfululizo kupanda Majukwaani kueneza Siasa za uongo, chuki na kutoridhika na matokeo.

Leo Baiden kashinda Urais USA hatujaona Trump na wenzake wapo barabarani wakiendeleza siasa na malumbano
 
Naunga mkono hoja, mama kaniuzi Sana KWA kauli yake ya jana juu ya vyama vya siasa, kawasha mtambo, inabidi sie wananchi kuuzima mapema kwa ili
 
Mikutano ya kisiasa hadharani sasa hv ya kazi gani mkuu? kama sio kuleta fujo tu!

Mama yupo sahihi kbs. Amani ndo kipaumbele. Kama katiba inasema tofauti basi iangaliwe upya!

Mikutano ya kisiasa hadharani ifanywe miaka ya uchaguzi
2024- Serikali za mitaa
2025- uchaguzi mkuu
 
Bado nina imani na mama! Pengine kapotoka kidogo lakini hajaharibu kabisa. Tumpe muda zaidi naye ni binadamu si mkamilifu. KUKOSEA KUPO!
Mshana, nakuapia Sasa tutaanza kushuhudia utekaji, mauaji, kubambikiwa kesi, upotezwaji na mengine mengi maovu ya Jiwe. Hii ni kauli ya kifo, maafa na maangamizi. Huyu mwanamke atakuwa hatari kuliko Magufuli nakwambia.

Sasa ukitaka kuanzisha chama utakienezaje? Huyu ni hatari Sana. Simpendi katu maana tunakwenda kufa
 
Hiyo Katiba iangaliwe upya, Mikutano ya kisiasa ISIWEPO mpaka muda wa Uchaguzi utakapofika.

Nchi zenye Demokrasia tangu miaka 200 iliyopita wanafanya siasa za hadharani inapokaribia Uchaguzi husika.

Sisi Tanzania tunataka miaka mitano mfululizo kupanda Majukwaani kueneza Siasa za uongo, chuki na kutoridhika na matokeo.

Leo Baiden kashinda Urais USA hatujaona Trump na wenzake wapo barabarani wakiendeleza siasa na malumbano
Wacha kudanganya, Trump kakusanya watu juzi kwa mikutano tu, na anaendelea na siasa wewe vp. Jamani nafikiri tujaribu kuheshimu na kufuata katiba zetu, hata kwa hii mbovu tuliyonayo.
 
Back
Top Bottom