nguruka wa kig0ma
JF-Expert Member
- Jan 16, 2020
- 2,946
- 2,932
Saalam,
Wewe ni Rais wa Watanzani wote, waliona vyama na wasionavyo walio na dini na wasio nazo. Wenye elimu, na wasio na elimu ambao ni wengi. Matajiri na masikini ambao ni wengi.
Wananchi wa Tanzania wanahitaji Katiba mpya ambayo itawahakikishia Uhuru wa kweli wa kuamua mambo yao na kupata haki zao.
Wapo wakubwa ndani ya chama chako hawataki kabisa kusikia neno katiba mpya au tume huru ya uchaguzi, wanajali matumbo yao na siyo ya masikikini walio wengi.
Alipoingia Magufuli watu wengi tulimtegemea na kutegemea kuwa atarejesha mchakato wa katiba iliyokwamishwa na CCM kwa masilahi yao.
Kuamini kule kulitokana na kama tuliona uchungu aliokuwa nao magufuli juu ya wanyonge na pesa za umma, kumbe alikuwa anatuchezea Karata tatu.
Tulio na akili nyingi tulipoona ameanza na kununua midege kwa pesa taslim,akaanza kujenga reli nk,tukajua katiba mp ya bye bye.
Nae alisema Kama ulivyosema wewe tofauti yenu ni sentensi tu,lakini maana ni moja.
NUKUU
Magufuli alisema Katiba mpya siyo kipaumbele chake. Tumuuache anyooshe nchi. Akasahau mabilioni ya fedha zetu zilizotafunwa kwenye kukusanya maoni na bunge la Katiba, ULE NI UFISADI
Wewe umesema tukuache urekebishe nchi. Je, jasho letu tulilovuja wakati tunatafuta pesa zilizokusanywa na kutumika kwenye mchakato ule limedondoka bure chini ya ardhi?
Kwa bahati mbaya sana watanzania wengi hawajui kuwa pesa zinazotumika na serikali zinatokana na wao,wangejua wangedai
Nakushauri
Yapo mambo ya kuwapendeza CCM, pia yapo mambo yakupasa kufuata matakwa ya wananchi bila kushauriwa. Turudishie rasimu ya Warioba ambayo ni maoni na matakwa yetu. Kwa kufanya hilo utakuwa umerekebisha nchi hii kizazi hiki na vizazi vijavyo.