Rais Samia, tafadhali usisaini marekebisho ya Sheria ya Kukata Watumishi 10% ya Mishahara. Huo ni mtego mbaya sana kwako

Rais Samia, tafadhali usisaini marekebisho ya Sheria ya Kukata Watumishi 10% ya Mishahara. Huo ni mtego mbaya sana kwako

JOSE KASANO

Senior Member
Joined
Apr 23, 2013
Posts
122
Reaction score
95
Inasikitisha sana kuona Bunge la Tanzania likipitisha Muswada wa marekebisho ya Sheria ya Mifuko ya Hifadhi ya Jamii kwa watumishi wa Umma kukatwa asilimia 10 ya mishahara yao kuchangia mifuko hiyo.

Kitendo hicho kitaleta athari kubwa sana kwa watumishi wa umma ambao wanachekelea kupandishwa mishahara na mama wakati fedha iliyoongezwa itakatwa kwa upande wa pili.

MADHARA YA SHERIA HIYO:
1. Madaraja ya mishahara waliyopewa watumishi na Dr. Samia yatakuwa sawa na bure.
2. Watumishi watajenga chuki na hasira dhidi ya serikali yao.
3. Fedha hiyo watakayokatwa hkun namna wataipata isipokuwa inapunguza mishahar yao na kuongeza ukali wa maish kwa watumishi wa umma.
4. Ikumbukwe mishahara haijaongezwa hivyo kwa watumishi na familia nyingi zikiwemo zile zinazotunzwa na watumishi hao itakuwa ni msiba mkubwa sana.
5. Morari ya kufanya kazi na kujituma kwa watumishi itashuka sana.
6. Kura za mama Samia zitaathirika sana kwa sababu tayari kwa watumishi kura zao zitakuwa rehani.

MWISHO, MAMA YETU KIPENZI, DR. RAIS NA AMIRI JESHI MKUU TAFADHALI USISAINI HYO MAREKEBISHO, YAFUTE UTARATIBU WA ZAMANI NDO UBAKI VILEVILE.

Kama ni hoja ya serikali kupunguza asilimi ya kuchangia kwenye mifuko ya hifadhi ya jamii kwa kila mtumishi ni mara mia moja serikali iondoe hiyo asilimia 5 ichangie 10% ni mtumishi achangie ileile iliyokuwepo badala ya kumbebesha mtumishi mzigo huo ambao inafahamika fika kabisa kuwa fedha hiyo mtumishi hataipata.

Soma No.10 yenye ammendment of section 12.
 

Attachments

Ofisi za serikali,baadhi ya watumishi hawawajibiki ipasavyo,wanakua wanainyonya serikali,mi kwa maoni yangu,mtendewe kama ITAKAVYO.
 
Hizo ni pesa zao hapo hasara iko wapi, siku zote mshahara hauwezi kutosha, mslalamiko ya mshahara ni kama ugonjwa usio pona.
 
Social security ni 20% - ratio ya mwajiri kwa mwajirisa kuchangia haitakiwi ipungue 50% kwa mwajiri.

Kwa wafanyakazi wa serikali kwa sasa wanachangia 5% na serikali (mwajiri) 15%

Kampuni nyingi za private ni 10% mwajiri 10% mwajiriwa.

Serikali imeamua kujipunguzia mzigo hivyo kuweni wavumilivu
 
CCM muendelee kushukuru kwa kuweka tume isiyo na uhuru wa kutenda haki kwa wapiga kura. Kinyume na hapo, kitambo sana mngekuwa mshaondoshwa kupitia sanduku la kura.
 
Back
Top Bottom