Akizungumza wakati akiendelea na ziara yake Mkoani Morogoro, Rais Samia amesema mbali na uzinduzi wa Miradi mbalimbali ya Maendeleo katika Mkoa huo, amefika pia kujionea hali ya Miundombinu ya Barabara iliyoharibiwa kutokana na Mvua za El Nino zilizonyesha kuanzia mwaka 2023.
Rais amesema Serikali imepata zaidi ya Dola Milioni 300 ambazo zitatumika kukarabati hali ya Barabara zote zenye changamoto ya kupitika baada ya kuharibiwa na Mvua.