McMahoon
JF-Expert Member
- Dec 22, 2017
- 1,353
- 1,639
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan,
Pole na majukumu ya kuongoza nchi na pia hongera kwa kazi nzuri unayofanya kuifanya nchi yetu inakua kiuchumi na kuwa na amani.
Kwa sasa dunia ni kijiji, unaweza kufanya kazi na mtu yoyote aliyeoko nje ya nchi.
Tuna tatizo la ajira kwahiyo vijana wengi wamekimbilia kujiajiri wenyewe na wengine kutoa huduma mtandaoni.
Ila ugumu unakuja kwenye kupokea malipo, tunahangaika sana. Nimekosa hela nyingi sana mpaka moyo unauma.
Mfano mtu yupo Ghana, India au Hungary anahitaji huduma yako na gharama yake ni fedha za kitanzania ni shiling 8,000 kila moja. Huyu mtu anahitaji kukulipa, atafanyaje ili akulipe? Sidhani kama mtu ataenda Western Union akutumie fedha yenye thamani ya shiling 8,000 za kitanzania.
Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan, tunahitaji usikie kilio chetu, uruhusu nasi, tupokee pesa kutoka paypal kama wanavyofanya wakenya. Wewe ni mama mwenye upendo, unawapenda wananchi wako na nchi yako. Na imani utasikia kilio chetu na utalifanyia kazi.
Kama wakenya wameweza, nasi tunaweza.