Nyakijooga
JF-Expert Member
- Dec 9, 2018
- 276
- 473
Mimi kazi zangu zinahusisha biashara chuma, bati n.k kwa ufupi vitu vinavyoendana na material hayo, ujumbe wangu huu uwafikie wahusika wa Shirika la Viwango Tanzania (TBS) na Wakala wa Vipimo (WMA), najua wao wapo kwa ajili ya kutusaidia Watanzania lakini inavyoonekana baadhi ya maafisa wao wanachofanya ni kama kushibisha matumbo yao.
Nasema hivyo kutokana na kinachoendelea kwenye Ulimwengu wa taaluma yetu hii, hawa Wamiliki wa viwanda vya Chuma na bati wengi wao wanatengeneza vitu vingi vyenye ubora wa chini.
Zamani bomba zilikuwa zina urefu wa Mita 6 au Futi 20 na ujazo wake ulikuwa mzito tofauti na ilivyo sasa.
Kwa sasa hata Mita 5 hazifiki, unakuta bomba in Sentimita 470 mpaka 480, hapo inategemeana na kiwanda, istoshe ni vyepesi kupita maelezo.
Swali ninalojiuliza hawa TBS hawajui haya yanayoendelea au wanachofanya ni kuangalia tu kwa macho bila kujali vipimo?
Nimemtaja Rais Samia kwa kuwa najua ana nguvu ya kutoa kauli kwa faida ya Taifa, watendaji wake wengi wa chini wakiwemo TBS na WMA, kwa kuwa najua baadhi ya Maafisa wao wanajua kila kitu kinachoendelea.
Upande wa nondo napo hali ni hiyohiyo, inatakiwa kuwa futi 40 lakini urefu haufiki huo, hakuna ubora mzuri, mizigo mingi imekuwa ikingizwa katika mzunguko lakini ubora wake haufai, matokeo yake tunajenga miundombinu isiyokuwa na ubora.
Hali hii inafanywa na viwanda vingi vilivyopo Dar es Salaam, mimi sisemi haya kwa kuwa nasikia bali kwa kuwa ndio maisha ninayoyaishi, ninafanya biashara na ninaona mizigo inayoingia na tunaowauzia wengi hawajui masuala ya ubora.
Nimeamua kusema hayo ili kuokoa Nchi yangu, kwani mimi nikianza kusema inamaanisha hata biashara yangu itakufa na ninaweza kuwa hatarini.
Wananchi wa kawaida hawajui ila mafundi wengi wanajua kinachoendelea lakini nao hawafanyi chochote kwa kuwa ndio ajira zao.
Namuomba Rais Samia atume watu wake wafuatilie kinachoendelea, inawezekana tukaona madaraja, nyumba na hata miundombinu ya ofisi ikichoka mapema au kuharibika mapema, lakini shida ni vifaa vilivyotumika wakati wa ujenzi.
Wito wangu kwa Rais Samia, elekeze ufanyike uchunguzi wa suala hili na baadhi ya maafisa wa taasisi hizo wachunguzwe kwa kuwa wengi wao wanaoingia ‘field’ kufanya ukaguzi wanajua kinachoendelea.
Pia soma ~ Wakala wa Vipimo (WMA) kufanya uhakiki wa Mita za Umeme, Maji na Mabando ya Simu