aishapatel
Member
- Nov 25, 2021
- 9
- 2
Ninaomba sana Mheshimiwa Rais na Serikali itupie jicho huduma zinazotolewa na RITA kwakweli wananchi tunazungushwa sana kupata huduma bila sababu za msingi.
Kwa sasa wameanzisha huduma ya kusajili vizazi na vifo kutumia mtandao lakini ukisajili maombi kupitia mtandaona kwenda HQ kufuatilia unapata usumbufu na watumishi wanakufokea kwanini ulisajili kupitia e-huduma,nani alikwambia utumie e-huduma kana kwamba kutumia huduma hii ni makosa makubwa.
Tafadhali kama huduma hii haiitajiki tunaomba ifungwe, Pili tunaomba kama hakuna staff wa kutosha kupokea simu za wateja tunaomba namba ya simu ifungwe badala ya kuwa haipokelewi au inakata yenyewe kabla ya mteja kusikilizwa.
vitu vidogo vidogo kama hivi vinavyosababisha mateso kwa wananchi ndio vinaleta mtazamo hasi kwa kazi kubwa ambayo serikali inafanya kutoa huduma kwa wananchi wake.
Naomba Serikali isikubali kukwamishwa na watu wachache wenye maslahi yao binafsi.
Naomba kuwasilisha