DOKEZO Rais Samia, Tusaidie NMB Bank mpaka leo hawajawalipa baadhi ya watumishi walioondolewa serikalini na hawana Mikopo

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Sir John Roberts

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Posts
12,835
Reaction score
23,584
Rais naamini upo kwaajili ya kutetea maslahi ya watu wa nchi hii. Uliamua watumishi wote waliotolewa kazini kwa matatizo ya vyeti walipwe stahili zao.

Napenda kukufahamisha kuwa hadi leo hii tarehe 7.03 2023 wapo baadhi ya waliokuwa watumishi wa serikali kupitia Bank ya NMB hawajalipwa fedha zao.

Nina ushahidi wa shemeji yangu tangu December mwaka jana PSSSF wanatuambia fedha imeshalipwa kupitia benki ya NMB lakini ukienda benki wanakwambia fedha hakuna mara utaambiwa mtandao unasumbua.

Kwakweli imekua ni kero tunaomba serikali iingilie kati kuwasaidia wananchi hawa.

Najua serikali ina mkono mrefu basi suala hili lichukuliwe kwa uzito wake..

Ahsante!
 
Benk ya NMB ifuatiliwe inakosa uadilifu kibiashara. Walipe fedha za watu.
 
Rais alipeleka NMB fedha za kuwalipia au NMB watoe hela yao ?

Lini tutapata wana taasisi wenye nguvu (wabunge, majaji, upinzani, civil society) za kuhoji na kupinga maamuzi kurupushi japo matamu matamu (populist) ya wanasiasa ?

Rais wa USA alitangaza msamaha kwa wadaiwa wote wa mikopo ya elimu. Baadhi ya wafia nchi wamepinga wakidai Rais kakurupuka, hajui consequences za amuzi lake. Kesi iko mahakamani, uamuzi umesitishwa.
 
Mtu umeghushi vyeti ili upate ajira. Umekaa katika ajira kimagumashi miaka nenda rudi huku wenye vyeti halali wakisota kitaa, umeshtukiwa ukaondolewa bila kufunguliwa kesi (kwasababu kiuhalisia wewe ni mwizi). Leo hii unalilia stahiki zako as if ni haki yako upewe [emoji848]
 
Malalamiko yako hayana msingi
 
Serikali ilikwisha peleka fedha za kulipa kwenye mabenki.
 
Kabla hujaomba msaada kwa Samia, kwanza tafuta wenzako ambao tayari wameshalipwa wakuthibitishie hilo, usiamini wanasiasa wakiwa kwenye mambo yao ya kisiasa..
 
Mtu umeghushi vyeti ili upate ajira. Umekaa katika ajira kimagumashi miaka nenda rudi huku wenye vyeti halali wakisota kitaa, umeshtukiwa ukaondolewa bila kufunguliwa kesi (kwasababu kiuhalisia wewe ni mwizi). Leo hii unalilia stahiki zako as if ni haki yako upewe [emoji848]
kauli ya raisi si ni sheria au!
 
Mtu umeghushi vyeti ili upate ajira. Umekaa katika ajira kimagumashi miaka nenda rudi huku wenye vyeti halali wakisota kitaa, umeshtukiwa ukaondolewa bila kufunguliwa kesi (kwasababu kiuhalisia wewe ni mwizi). Leo hii unalilia stahiki zako as if ni haki yako upewe [emoji848]
Uamuzi ulishatoka kwamba walipwe, sasa sijui hiki kinachokuwasha ni nini hasa....
 
Nina mashaka kama shida ni NMB. Mifuko ya hifadhi za jamii kuna mambo ya ajabu sana, na serikali haiwezi kufanya kitu kwasababu wao ndio chanzo kikuu cha matatizo ya kifedha kwenye hiyo mifuko.
 
Mtu umeghushi vyeti ili upate ajira. Umekaa katika ajira kimagumashi miaka nenda rudi huku wenye vyeti halali wakisota kitaa, umeshtukiwa ukaondolewa bila kufunguliwa kesi (kwasababu kiuhalisia wewe ni mwizi). Leo hii unalilia stahiki zako as if ni haki yako upewe [emoji848]
Kwa hiyo wewe mfanyakazi wa NMB unazuia malipo ambayo yametolewa na serikali na unataka wasidai au kulalamika?

Je hujui kuna nchi watu wanafungwa jela kwa uhalifu na wakitoka wanapewa pesa ila aanze maisha?

Je unajua scenario ya kughushi vyeti ilivyokuwa na double standards?Kuna watu ni mawaziri leo wana PhD na walighushi vyeti au majina ya kidato cha nne?Je unamkubuka profesa wa jalalani naye jina lake lilitoka ameghushi cheti?
Kuna daktari bingwa wa upasuaji ( ni bingwa kweli) jina lilitoka kwenye orodha ya walioghushi vyeti.Waulize waliosoma udaktari Muhimbili zamani hizo iwapo ingekuwa rahisi kupenya ukiwa kilaza.Na huyu hadi masters ya surgery amesoma Muhimbili.

Kuna watu waliondolewa kwa kuonekana ameghushi cheti kutokana na kurudia darasa la saba kwa jina la mtu mwingine na baadae huko mbele akabadili jina bila utaratibu kurudia jina lake na amesoma hadi masters na alifaulu kote huko tangu advance.

Tatizo la watu wengi hawawezi kufikiri ndio maana wanahukumu kirahisi.Kuna watu walighushi majina tu lakini walikuwa na akili kuliko wewe hapo na wamelitimikia taifa kwa uaminifu
 
Hawa vijana wa dot.com hawawezi kuelewa.......zamani nafasi za kwenda sekondari zilikuwa finyu sana na zilikuwa na figisu nyingi hivyo ilikuwa kawaida watu kurudia darasa la saba kwa majina ya watu wengine hususani wale walioacha shule, siyo kwamba walikuwa vilaza ila nafasi zilikuwa finyu. Sasa watu wazima kama huyo daktari bingwa, kabudi au hata madelu kukumbwa na dhahama ya majina haimaanishi kwamba walikuwa vilaza, ni mazingira tu ukichukulia pia wengi wao enzi hizo wametokea mazingira duni ya vijijini.​
 
Kwa hiyo wewe mfanyakazi wa NMB unazuia malipo ambayo yametolewa na serikali na unataka wasidai au kulalamika?

Je hujui kuna nchi watu wanafungwa jela kwa uhalifu na wakitoka wanapewa pesa ila aanze maisha?

Je unajua scenario ya kughushi vyeti ilivyokuwa na double standards?Kuna watu ni mawaziri leo wana PhD na walighushi vyeti au majina ya kidato cha nne?Je unamkubuka profesa wa jalalani naye jina lake lilitoka ameghushi cheti?
Kuna daktari bingwa wa upasuaji ( ni bingwa kweli) jina lilitoka kwenye orodha ya walioghushi vyeti.Waulize waliosoma udaktari Muhimbili zamani hizo iwapo ingekuwa rahisi kupenya ukiwa kilaza.Na huyu hadi masters ya surgery amesoma Muhimbili.

Kuna watu waliondolewa kwa kuonekana ameghushi cheti kutokana na kurudia darasa la saba kwa jina la mtu mwingine na baadae huko mbele akabadili jina bila utaratibu kurudia jina lake na amesoma hadi masters na alifaulu kote huko tangu advance.

Tatizo la watu wengi hawawezi kufikiri ndio maana wanahukumu kirahisi.Kuna watu walighushi majina tu lakini walikuwa na akili kuliko wewe hapo na wamelitimikia taifa kwa uaminifu
Asante sana kwa kumueleza ukweli
 
Mtu umeghushi vyeti ili upate ajira. Umekaa katika ajira kimagumashi miaka nenda rudi huku wenye vyeti halali wakisota kitaa, umeshtukiwa ukaondolewa bila kufunguliwa kesi (kwasababu kiuhalisia wewe ni mwizi). Leo hii unalilia stahiki zako as if ni haki yako upewe [emoji848]
Walitumikia nchi katika utumishi wao pia.
 
Back
Top Bottom