Rais Samia tuwe wawazi, uteuzi wa Mwigulu ulichemka

BestOfMyKind

JF-Expert Member
Joined
Apr 26, 2012
Posts
1,350
Reaction score
1,464
Dude is very smart bookwise ila wizara ya fedha sio mahali pake. Wizara ya fedha inahitaji a practising economist. Mwigulu uchumi aliuweka kando zamani siku hizi amekuwa mwanasiasa. Hapa ilitakiwa aina ya watu kama hayati Dr. Mgimwa au Makamu wa Raisi Dr. Mpango. Serikali inawajua watu wengi ambao ni practising economists sijui kwanini mmemuweka mwanasiasa. Tujifunze kwa wenzetu walioendelea kwasababu mambo ya uteuzi hayajaanzia kwetu.

Nasikia mfumo wa ukusanyaji mapato wa serikali kwa njia ya Control Number haufanyi kazi sasa hivi kwa zaidi ya mwezi mmoja. Huu mfumo ndio uliowezesha kupungua kwa wizi wa fedha za umma, maana risiti ya malipo unapata palepale unapolipia na fedha zote zinaenda hazina kabla ya kurudi kwenye taasisi husika. Ukifungwa huu maana yake watu wataaanza kukusanya hela za umma mikononi na upigaji utarudi tutrudi miaka 10 nyuma.

Mimi sikupangii cha kufanya Mheshimiwa ila una uwezo mkubwa wa kupata taarifa sahihi, zitumie tafadhali. Tumechoka kuwa kwenye nchi ambayo hata ufanyeje uwezo wa kifedha wa mtu mmoja hauwezi kuzidi dola za kimarekani billioni 10. Nchi yetu bajeti yake kwa mwaka ni kati dola billioni 10 hadi dola billioni 15, hii sio sawa.

Kuna watu wanazaliwa bila hela wana fught mpaka anakuwa na uwezo wa kuingiza tsh milioni 100 kwa mwezi consistently, lakini kwasababu ya uchumi mdogo hapo ndio inakua kikomo chake. Tungekua na uchumi imara hii nchi ingekua na mamimilionea wa dollar wengi sana.

Muhamishe wizara Mwigulu tafadhali, kuna wachumi wazuri sana nchi hii teua mmoja uchumi upae. Ni aibu wataalamu wa uchumi wa Tanzania wanaenda kushauri nchi kama South Africa, mashrika kama IMF na WB kuhusu kupunguza umasikini wakati nchi yetu sisi bado masikini.

Pata watu ambao wataongeza pato la taifa kwa kuchochea biashara za nje ya nchi. Tutapata hela za ziada ambazo hazipo kwenye mzunguko na bajeti yetu itakua. Sio mtu anataka kuongeza kodi juu ya VAT ambayo watu wanakatwa bila hiari yao.

Wizara nyingine hizo sawa ila hii inahitaji msomi, Marekani kuna mama amabe ni kiongozi wa idara ya fedha. Mama yule tokea ameanza kwenda shule yeye anawaza uchumi tu, ana phd za uchumi na ameandika vitabu vya kutosha kuhusu uchumi. Sisi masikini huku mnatuwekea mwanasiasa mwenye masters ya uchumi hapo UDSM.

Inatakiwa twende kwa kasi na Mwigulu sio mmoja wa watu wanaotakiwa kwenye wizara ya fedha.
 
Nilidhani ni mimi tu nisiye na imani nae kwani ni mtu wa jeuri na majivuno analazimisha mambo anavyotaka.

Kaongeza mikodi bila kutafakari wananchi watalipia kodi hizo kutoka wapi.

Wizara nyeti sana aliyonayo ila haiwezi kabisa hataki ushauri na hasiki malalamiko wala maoni ya wananchi.

Kaanzisha adhabu ya kulipia leseni za biashara mara mbili mtu anapochelewa kurenew na bado hasikii wala haelewi.

Hivi kweli mtu kachelewa mwezi mmoja kurenew leseni ya biashara ya Tshs. 81,000/= unamlazimisha kulipia 162,000/= ambapo unadai ni adhabu?

Rais ondoa hii mtu imeshindwa wizara.
 
Kwenyd makadirio ya kodi TRA ndio balaa.mtaji laki nane kodi laki moja na nusu!
 
Kama kweli mfumo wa malipo haufanyi kazi kwa mwezi mmoja, hii si bahati mbaya, hata mtaani huku siku hizi kuomba risiti unaonekana mshamba, na muuzaji anakataa kutoa risiti kibabe tu bila woga.

Ni ajabu sana kwa awamu hii, malalamiko yamekuwa yakielekezwa moja kwa moja kwa wahusika tofauti na hapo nyuma kuwa kila linaloharibika/linaloharibiwa lilielekezwa kwa raisi, inapaswa kuwa hivi wakati wote.

Dhana moja nzuri ni watendaji wote chini ya raisi kufanya kazi, ama kwa hiari au kwa kulazimika kwa misingi ya utumishi, ama kwa kumuogopa raisi au kuheshimu mamlaka na si kinyume chake.

Nimeanza kuelewa kwanini JPM alianza kuteua teua watu nje ya chama.

Mwigulu hajawahi kufaa popote pale alipowahi kuwekwa, Simbachawene kadhalika, Masauni, Mwinyi, Uwesu/o n.k Wengine pia walionekana watendaji kwasababu ya msimamizi wao, Kalemani, PM, aliyekuwa waziri wa fedha, Doto, Aggrey, n.k

Hivi haiwezekani, mathalani, pengine uteuzi ukawa unafanana kwa karibu na ubobevu wa eneo husika, sio tu kitaaluma, pia kwa uzoefu wa field? Waziri wa ulinzi akawa ni general mstaafu aliyefanya vizuri enzi zake bila makando kando, n.k!
 
Huyu Madelu si ndio alitoa hela kwa vijana wake waandike mawe yote Tanzania Mwigulu Rais 2020...?,

Na anavyo vaa tai ya bendera ya Tanzania anatuona wananchi wengine wote ni matakataka.

Jana kaongea hoja za kipuuzi sana Clouds, Me i wonder Serikali inakuaje na wabunge wenye glimpase view kama huyu na ni Waziri sekta nyeti. Na wale waliokuwa wanamuhoji ni kama walikua wana vizia teuzi wana muogopa ogopa kumpigisha HardTalk za moto sana mpaka ajute kuhojiwa live. Waandishi wale walitakiwa wampige maswali magumu sana mpaka abaki anazunguruka kwenye kiti kiwe hakikaliki ...sasa maswali mepesi mepesi af anajibu kwa kulegeza sauti na anajibu utopolo.

Et tumeongeza sh 100 kwenye kila lita ya mafuta, mbona huwa yana pandaga na hatulalamiki.. like seriously?? Halafu anakataa kuwa Zambia mafuta hayo hayo ni bei rahisi kuliko Dar na wakati yanatoka Dar.. huyu mtu mtoeni hapo.

Itafika hatua watu watatoka Mbeya mjini kwenda Zambia Nakonde kujaza mafuta na madumu na wanarudi zao Mbeya wasione hasara ya kilometa 200 za kwenda na kurudi.. ikiwa kwa sasa hivi watu wameanza kutoka Tunduma kwenda Nakonde kujaza fulltank na kurudi, bei ya petroli kule ni 1850 kwa lita. Wakati Tunduma ni 2500+ huu ni UPUMBAVU na aibu kwa nchi na viongozi wake.

Mtu heshimu wananchi na kodi zetu. Hizo kodi mnazo jiamulia kuweka... mpaka kwenye miamala ya simu kwani kodi mnazotukata na mlizokuwa mnatukata tangu zamani zilikuwa zinafanya kazi gani,?
 
Umeandika kimajungu sana mkuu ujue pia kuwa waziri ni mwanasiasa pale wizarani yeye ni kama kiongozi tu lakini kuna wataalamu wa uchumi pale ambao wanaandaa kila kitu Nchemba yeye anapikiwa kila kitu hawezi kutengeneza kila kitu yeye pale wizarani wapo wanaomtengenezea labda ungesema kuwa waifumue wizara nzima hapo sawa lakini kumlaumu mwanasiasa?utakuwa unaleta majungu tu mkuu
 
unajuwa mnapoandika msiandike kiushabiki tu jamani mimi nalipia malipo kwa control numba kila siku sasa huko amabko control number haifasnyi kazi ni wapi?
 
Huyu na wale wa wizara ya mahusiano na teknolojia,mama anatuangusha!
Labda anavuta kasi atawatoa tu tujipe muda
 
yani umeongea jambo la maana kweli, watu wakienda kujaza mafuta zambia hela zetu zinahama nchi. Na mafuta watu wanajaza kila siku kwahiyo tunapoteza hela nyingi sana. Mwisho wa siku bajeti ikipangwa inaonekana haitoshi wanaongeza ushuru tena kumbe wachawi ni sisi wenyewe.
 
Umeandika kimajungu sana mkuu ujue pia kuwa waziri ni mwanasiasa pale wizarani yeye ni kama kiongozi tu lakini kuna wataalamu wa uchumi pale ambao wanaandaa kila kitu Nchemba yeye anapikiwa kila kitu hawezi kutengeneza kila kitu yeye pale wizarani wapo wanaomtengenezea labda ungesema kuwa waifumue wizara nzima hapo sawa lakini kumlaumu mwanasiasa?utakuwa unaleta majungu tu mkuu
sera za wizara zinaongozwa na Waziri hakuna jungu hapo. Kama waziri anapokea ushauri wa kuongeza ushuru juu ya VAT na akaukubali ujue yeye ndio tatizo. Mtaalamu wa uchumi hawezi kusimamia sera zinazodidimiza uchumi. Hili swala liangalie objectively, mimi sio mpinzani wa serikali, naipenda nchi yangu saaaaaaaana.
 
unajuwa mnapoandika msiandike kiushabiki tu jamani mimi nalipia malipo kwa control numba kila siku sasa huko amabko control number haifasnyi kazi ni wapi?
umelipia nini kwa control namba na ni lini? kuna tofauti kati GePG kiujumla na control number
 
Back
Top Bottom