Huyu Madelu si ndio alitoa hela kwa vijana wake waandike mawe yote Tanzania Mwigulu Rais 2020...?,
Na anavyo vaa tai ya bendera ya Tanzania anatuona wananchi wengine wote ni matakataka.
Jana kaongea hoja za kipuuzi sana Clouds, Me i wonder Serikali inakuaje na wabunge wenye glimpase view kama huyu na ni Waziri sekta nyeti. Na wale waliokuwa wanamuhoji ni kama walikua wana vizia teuzi wana muogopa ogopa kumpigisha HardTalk za moto sana mpaka ajute kuhojiwa live. Waandishi wale walitakiwa wampige maswali magumu sana mpaka abaki anazunguruka kwenye kiti kiwe hakikaliki ...sasa maswali mepesi mepesi af anajibu kwa kulegeza sauti na anajibu utopolo.
Et tumeongeza sh 100 kwenye kila lita ya mafuta, mbona huwa yana pandaga na hatulalamiki.. like seriously?? Halafu anakataa kuwa Zambia mafuta hayo hayo ni bei rahisi kuliko Dar na wakati yanatoka Dar.. huyu mtu mtoeni hapo.
Itafika hatua watu watatoka Mbeya mjini kwenda Zambia Nakonde kujaza mafuta na madumu na wanarudi zao Mbeya wasione hasara ya kilometa 200 za kwenda na kurudi.. ikiwa kwa sasa hivi watu wameanza kutoka Tunduma kwenda Nakonde kujaza fulltank na kurudi, bei ya petroli kule ni 1850 kwa lita. Wakati Tunduma ni 2500+ huu ni UPUMBAVU na aibu kwa nchi na viongozi wake.
Mtu heshimu wananchi na kodi zetu. Hizo kodi mnazo jiamulia kuweka... mpaka kwenye miamala ya simu kwani kodi mnazotukata na mlizokuwa mnatukata tangu zamani zilikuwa zinafanya kazi gani,?