ChoiceVariable
JF-Expert Member
- May 23, 2017
- 66,537
- 75,687
"Niwaombeni chaguzi zinazokuja hizi elekeeni kwenye maendeleo, waswahili wanasema anayekufaa kwa dhiki ndiye nani? sasa ntakushangaa una rafiki mzuri ndani ya nyumba yako anayekufaa kwa dhiki zote, kula, kuvaa na yote, unakwenda kwa rafiki mwingine nje ya nyumba yako ambaye hakufai kitu au anataka uchukue anachokileta rafiki yako wa nyumbani umpe yeye" - Rais Samia
===
Naunga mkono hoja hii,sio wakati wa neema ndio watu wanajitokeza kujifanya wema tena wanakuja na msimulizi matamu ila wakati wa shida walikuwa wanawacheka eti mkome.
Nadhani Wananchi wa Tanzania wameelewa vyema ujumbe wa Mh.Rais na hawatafanya kosa Mwaka 2024 &2025.
My Take
Kila mtu atakula kule anakopeleka unga na ataota moto na wale ambao walisenya Kuni pamoja.