Rais Samia umeupiga mwingi kwenye Utumishi wa Umma, ila kuna moja linaloumiza utumishi wa umma umeliacha

Rais Samia umeupiga mwingi kwenye Utumishi wa Umma, ila kuna moja linaloumiza utumishi wa umma umeliacha

mkamanga original

JF-Expert Member
Joined
Jan 21, 2015
Posts
637
Reaction score
663
Rais wetu umejitahidi kufuta maumivu ya watumishi Wa umma wa nchi hii pamoja na makundi mengineyo yaliyokuwa yameathirika na utawala wa JPM.

Hakika katika utawala Wa mwendazake wananchi wameona rangi mbalimbali

Magufuri aliweka utaratibu mbaya Wa upandaji Wa madaraja ya mishahara pamoja na vyeo kwa watumishi Wa umma. Utaratibu uliokuwepo tangu tawala zilizopita ilikuwa kila baada ya miaka 3 mtumishi Wa umma alikuwa anapanda daraja nchi nzima sekta zote ilikuwa hivyo, mtumishi alikuwa hivyo.

Mwendazake alibadilisha utaratibu na kufanya mtumishi Wa umma alilazimika kukaa miaka 5 kwenye daraja moja baadala ya miaka 3 utaratibu aliokuta.

Utaratibu huu unaumiza sana maisha ya watumishi.

Mtumishi Wa umma analazimika kukaa miaka 15 ili awe mwandamizi,wakati huko nyuma mtumishi alikuwa anakaa miaka 7, alikuwa anatosha kuwa mwandamizi.

Tunaomba utaratibu ubadilike unaumiza watumishi. Turudishe kule tulikotoka miaka 7 mtumishi aliyefanya kazi kwenye field moja anao uzoefu Wa kutosha kuwa mwandamizi na sio hiyo 15 ambayo mwendazake ametuachia, utaratibu uwe kila baada ya miaka 3 mtumishi anapanda daraja baada hii ya sasa.

Hapo zamani mtu akishafanya kazi miaka 7 inatosha kabisa kuwa na uzoefu Wa kutosha katika field yake na kuwa mwandamizi,na hata katika vyeo alitosha kabisa kufanyiwa vetting na kushika nafasi za kioungozi,lakini sasa ni ngumu kwa utaratibu huu Wa mwendazake
 
Mbona bado ni mitatu+1. Hiyo plus 1 maanake ni ule wa matazamio kabla ya kuwa confirmed.
 
Kama una uhakika regime ya JPM ilifanya mabadiliko, tunaomba waraka au hata tangazo la gazeti(GN). Au unampakazia tu mzee wa watu? Hivi mtaweka wapi nyuso zenu nyakati zijazo? Hakuna kidumucho jamani. Vitu vyote vyapita. Msijisahau sana.
 
Kama una uhakika regime ya JPM ilifanya mabadiliko, tunaomba waraka au hata tangazo la gazeti(GN). Au unampakazia tu mzee wa watu? Hivi mtaweka wapi nyuso zenu nyakati zijazo? Hakuna kidumucho jamani. Vitu vyote vyapita. Msijisahau sana.
Anachosema ni kweli mwenyewe ni nimewahi ajiriwa nikakaa miezi 9 nikajitoa
 
Utumishi wa uma kwa sasa😁😁😁

Uk.jpg
 
Back
Top Bottom