Mr Dudumizi
JF-Expert Member
- Sep 9, 2020
- 7,799
- 14,215
Kwa heshima na taadhima mama yetu wa Taifa, mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu wa majeshi yote ya ulinzi na usalama napenda kwanza kukusalimu "Kwa Jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania". Ama baada ya salam napenda kutumia nafasi hii kama mtanzania na raia mwema wa nchi yako pendwa ya Tanzania kukushauri mambo fulani, lakini kwa kupenda kwako unaweza ukauchukua ushauri huu wote au baadhi au ukaachana nao kwa jinsi utakavyoona mwenyewe inafaa.
(1) Kitu cha kwanza kabisa ningependa kukushauri mh raisi ni kufuata na kuikamilisha ilani ya chama chenu mliyoahidi kuitekeleza wakati wa kampeni. Mfano kuna miradi mikubwa, yenye tija na faida kubwa kwa nchi ambayo aliekuwa raisi wetu hayati Magufuli alifariki bila kuimaliza, ni vizuri ukaimaliza tena kwa wakati uliopangwa ili wale wananchi wanao nufaika na miradi hiyo waweze kukuchagua au kukichagua tena chama chako mwaka 2025.
Na kumbuka ilani ndio msingi au muongozo wa serikali yoyote iliyopo madarakani, ina maana serikali inayoacha kufuata ilani ya chama chake iliyoahidi mbele ya wananchi, inakuwa kama vile treni inayoacha reli na kutembelea kwenye mchanga. Kwahiyo wewe kama raisi na mwenyekiti wa chama chenu jitahidi sana ukamilishe ahadi ya ilani ili iwe rahisi kuaminiwa tena na wananchi mwaka 2025, na hatimae chama chenu kupata ushindi mnono zaidi ya huu mlioupata mwaka 2020.
(2) Ruhusu mikutano ya vyama vya siasa kwa mujibu wa katiba, lakini vyama hivyo vifanye mikutano yao kwa kufuata sheria, sio mwanasiasa anakosa hoja au sera nzuri za kuwaeleza wanachama wake anaanza kudandia majina ya watu kwa kuwashutumu ufisadi bila kuwa na ushahidi wa tuhuma zake (kama ilivyotokea kwa mh Lowasa, Sumaye nk) unakuta anashutumiwa mtu ufisadi bila ushahidi akienda kuripoti polisi yule mwanasiasa akikamatwa kwa kukosa ushahidi wa tuhuma zake, wafuasi wake wanaingia barabarani kuandamana eti kiongozi wao kaonewa nk.
(3) Lisimamie mwenyewe swala la ajira ili kila anaestahili kupata ajira aipate kwa haki bila kuangaliana undugu, urafiki, ukabila, udini na ukanda.
(4) Simamia haki bila kuangalia huyu anasema nini radioni, gazeti au mitandaoni, maana katika vitu ambavyo huhatarisha usalama wa nchi basi mitandao nayo imo, kwahiyo ni kuwa makini sana na taarifa za mitandaoni.
(5) La mwisho nashauri mh raisi ufanye uteuzi kulingana na taaluma ya mtu ili kuleta ufanisi katika kazi zao. Sina mengi zaidi ya hayo, ni mimi raia wako mwema mr D. Kwa niaba ya TAKWA au kwa kirefu chake "Tanzania Kwanza"