Pre GE2025 Rais Samia utashinda Uchaguzi Mkuu 2025 lakini rekebisha hili

Pre GE2025 Rais Samia utashinda Uchaguzi Mkuu 2025 lakini rekebisha hili

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Samiaagain2025

JF-Expert Member
Joined
Dec 2, 2020
Posts
3,626
Reaction score
3,869
Nakupongeza kwa moyo wa dhati kwa kupitishwa na chama chetu kuwa mgombea urais na ndipo utakuwa rais wa JMT 2025-2030.

Kuna jambo ambalo sisi tukupendao kwa dhati na wenye kulipenda Taifa letu lazima tukuambie ukweli.
Jambo lenyewe ni hili la utekaji na mauaji ya raia; ambao kwa kiasi kikubwa wana mlengo wa kupinga au kukosoa serikali.

Naomba nikukumbushe mpendwa Rais wangu kuwa MUNGU anachukia sana kitendo cha binadamu kumtoa uhai binadamu mwingine, tena kwa kile ambacho kingeepukika.

Sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani nkuomba ukomeshe hili jambo na ikiwezekana wahusika wa moja kwa moja tuwajue ili wawajibishwe kisheria.

Kwenye katiba yetu hakuna kipengele KINACHOMPA mtu yeyote mamlaka ya kuua( isipokuwa ktk mazingira fulani hivi mf.kwenye vita, kujihami n.k). Jitahidi uwe na kauli ya mwisho kwenye jambo hili.

Mheshimiwa rais, Kwa mfano uliwahi kuagiza vyombo vya ulinzi na usalama vichunguze mauaji na kutekwa kwa mtu mmoja, mwezi Septemba mwaka jana.

Sijui kama uliowaagiza wameshakamilisha au la.
Na pengine sio lazima kutangaza hadharani taarifa ya uchunguzi huo.

LAKINI hii ni aibu kwa Taifa letu ambalo hatukuwa na utamaduni huu tangu kuasisiwa. Nimekuandikia haya kwa sababu nakupenda wewe na TAIFA langu.

NAKUTAKIA USHINDI MWEMA.

MUNGU IBARKI TANZANIA.
 
Unamtakia ushindi Samia wakati kuna utekaji na mauaji yanaendelea serkalini?!
 
Unataka tukujibu vipi wakati chadema bado haijakamilisha safu yao ya uongozi kuelekea uchaguzi mkuu? Labda atashinda ukimlinganisha na wale ambao nao tayari wamekamilisha wagombea wao wa urais.
 
Unataka tukujibu vipi wakati chadema bado haijakamilisha safu yao ya uongozi kuelekea uchaguzi mkuu? Labda atashinda ukimlinganisha na wale ambao nao tayari wamekamilisha wagombea wao wa urais.
Mkuu huu ujumbe ni wa Mgombea wa chama Chake
 
Nakupongeza kwa moyo wa dhati kwa kupitishwa na chama chetu kuwa mgombea urais na ndipo utakuwa rais wa JMT 2025-2030.

Kuna jambo ambalo sisi tukupendao kwa dhati na wenye kulipenda Taifa letu lazima tukuambie ukweli.
Jambo lenyewe ni hili la utekaji na mauaji ya raia; ambao kwa kiasi kikubwa wana mlengo wa kupinga au kukosoa serikali. Naomba nikukumbushe mpendwa Rais wangu kuwa MUNGU anachukia sana kitendo cha binadamu kumtoa uhai binadamu mwingine, tena kwa kile ambacho kingeepukika.
Sasa tunapoelekea kwenye uchaguzi mkuu wa rais, wabunge na madiwani;
nakuomba ukomeshe hili jambo na ikiwezekana wahusika wa moja kwa moja tuwajue ili wawajibishwe kisheria.
Kwenye katiba yetu hakuna kipengele KINACHOMPA mtu yeyote mamlaka ya kuua( isipokuwa ktk mazingira fulani hivi mf.kwenye vita, kujihami n.k).
Jitahidi uwe na kauli ya mwisho kwenye jambo hili.

Mheshimiwa rais, Kwa mfano uliwahi kuagiza vyombo vya ulinzi na usalama vichunguze mauaji na kutekwa kwa mtu mmoja, mwezi Septemba mwaka jana.
Sijui kama uliowaagiza wameshakamilisha au la.
Na pengine sio lazima kutangaza hadharani taarifa ya uchunguzi huo.
LAKINI
hii ni aibu kwa Taifa letu ambalo hatukuwa na utamaduni huu tangu kuasisiwa. Nimekuandikia haya kwa sababu nakupenda wewe na TAIFA langu.

NAKUTAKIA USHINDI MWEMA.

MUNGU IBARKI TANZANIA.
Wewe umekomaa kisiasa na ni mkweli sio kina Lukas Mwashambwa na dada yake tlaahtlaah ni kupamba tuu hata chooni!
 
Ndugu Lice hilo sahau! Anayajua hayo mambo sana ila hana cha kufanya.
 
Back
Top Bottom