Rais Samia; Wakulima wanalia sana na bei ya mbolea, ni Kama hawasikikizwi

Memento

JF-Expert Member
Joined
Jun 13, 2021
Posts
4,423
Reaction score
9,986
Mama Samia ukweli ulio wazi kabisa ni kuwa watanzania walio wengi ni wakulima.

Hapa nazungumzia 70% ya watanzania wote, hebu jionee jinsi hili kundi lilivyo na watu wengi kuliko shughuli nyingine yoyote.

Bei ya mbolea ni kilio na kilio tena, Hawa wakulima walio wengi hata umeme hawajui upoje wao ni jembe, jembe na wao.

Weka nguvu huku, wasaidie hawa. Jana nilikuwa songea, wakulima wanalia sana na bei.

Hii Bei hawajawahi kuishuhudia katika maisha yao, ni kilio tu.

Mama Samia Kama itakupendeza weka ruzuku kwenye mbolea ili Bei ishuke uwasaidie hawa.

Walizoea kununua UREA kwa 50,000 Leo wanainunua 100,000.

Fanya Jambo huku mama
 
Huyu Samia ni kolo wa kutupa! Anavuna mabilioni kwenye tozo za muamala lakini ameona haitoshi akaamua kufuta ruzuku kwenye mbolea[emoji34]

Lakini hii nimeipenda, unajua makulima mengi ni maccm, so acha dawa iwaingie
 
Acha kumtusi Mh.Rais, Msukuma wenu aliharibu mifumo ya nchi then unamsingizia mama ambaye ameishia kubeba burden bureeee!
Ngoja tumchague nayeye 2025 then tutamu-assess kwa sera zake, sheria zake na misimamo yake, tulia tujenge nchi!
 
Hicho Chama cha Wakulima na Wafanyakazi kimegeuzwa kuwa cha Waiba Kura na Watekaji.
 
Wakulima wadogo wadogo wa tz wengi n CCM

Bei haitoshi SSH ongeza ifike 350k akili ziwakae vizuri

Utawasikia wapinzan tukiwapa nchi had wajenge ikulu Yao na jeshi lao had lini acha akili ziwakae
 
Hii Nchi Haina Mawaziri?

Waziri Mkuu wa Taifa Stars

Rais atafanya mangapi?

Kilimo...na ufugaji umedorora...

Utalii hauponi, Coronavirus iliathiri utalii, na Waziri wa utalii Hana wazo la Nini kifanyike...huyu ni Lawyer by professional..je wataalamu wanampotosha?

Afadhali Kigwangala arudi kwenye utalii, au naibu wake Kanyasu.

Ilani ya CCM inasema watalii million 5, kabla ya 2025...hakuna dalili.

Tunakwama wapi?

@kigwangala

mwigulu
 
17 machi watanzania wanyonge walipigwa na nondo ya mm 30 kichwani. Chaliiiiiii
 
Mama Samia ukweli ulio wazi kabisa ni kuwa watanzania walio wengi ni wakulima.

Hapa nazungumzia 70% ya watanzania wote, hebu jionee jinsi hili kundi lilivyo na watu wengi kuliko shughuli nyingine yoyote.

Bei ya mbolea ni kilio na kilio tena, Hawa wakulima walio wengi hata umeme hawajui upoje wao ni jembe, jembe na wao.

Weka nguvu huku, wasaidie hawa. Jana nilikuwa songea, wakulima wanalia sana na bei.

Hii Bei hawajawahi kuishuhudia katika maisha yao, ni kilio tu.

Mama Samia Kama itakupendeza weka ruzuku kwenye mbolea ili Bei ishuke uwasaidie hawa.

Walizoea kununua UREA kwa 50,000 Leo wanainunua 100,000.

Fanya Jambo huku mama

Tatizo la mbolea ni uagizaji na ndiyo wanajenga kiwanda. Bei imepanda Dunia nzima inabidi kiwanda kiishe haraka.
 
Kilombero mbolea ilipanda mara tatu ndani ya wiki moja,,, i mean ndani ya siku saba yaan ata stock stoo bado haijaisha mtu anajiamulia tu,. Tsh67, 000 - tsh 84,000 - tsh98, 000.

Wakati huo huo gunia la mpunga ni 70k-80k
 
Huyu Samia ni kolo wa kutupa! Anavuna mabilioni kwenye tozo za muamala lakini ameona haitoshi akaamua kufuta ruzuku kwenye mbolea[emoji34]

Lakini hii nimeipenda, unajua makulima mengi ni maccm, so acha dawa iwaingie
Ruzuku kwenye mbolea alifuta magu
 
Back
Top Bottom