Rais Samia wakumbuke waalimu

Rais Samia wakumbuke waalimu

Lotus 123

JF-Expert Member
Joined
Nov 5, 2021
Posts
3,151
Reaction score
5,513
Hadhi ya kazi ya ualimu inashuka sana, naomba walimu wapewe kipaumbele kwenye maslahi yao, hata hiyo mishahara ipande pande kidogo.

Tatizo la kada hii nje na mshahara hakuna plan B, hakuna posho, madaraja yenyewe kupanda miaka mitano, mtu akipanda mara nne kazeeka.

Wewe fikiria mtu anaanza kazi na miaka 30, kupanda daraja miaka 5, akipanda mara nne tayari ni Mzee na mishahara yenyewe ndiyo hiyo kiduchu.

Wahanga wakubwa ni walimu wa kike, imagine madam anaolewa na boda boda, au anakuwa na madeni kila mahali, unafikiri kuna mtoto anakuwa na morali asome?
 
Back
Top Bottom