Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 19,362
- 48,879
Mh. Rais, umekamilisha teuzi za wakuu wa mikoa na wilaya. Na sasa bado nafasi za wakurugenzi wa Halmashauri, miji, manispaa na majiji.
Teuzi zilizotangulia, zilikuwa ni teuzi za ulaji na shukrani kwa sababu kimsingi wakuu wa wilaya na mikoa, tangu enzi za mkoloni, walitumika kama vikaragosi wa mtawala. Kazi yao kubwa ilikuwa kulinda maslahi ya mtawala na siyo wananchi. Hali hiyo, kwa kiasi kikubwa imebakia kuwa hivyo mpaka leo, ndiyo maana wananchi wengi wenye uelewa, wangependelea nafasi hizi zifutwe.
Sasa zimebakia nafasi za wakurugenzi. Hizi ni nafasi muhimu sana maana zinahusu maendeleo ya wananchi. Hizi ni nafasi za kitaalam na kiutendaji. Ndiyo maana sheria zinamwelekeza Rais kuteua wakurugenzi kutoka miongoni mwa watumishi wa umma waliofikia daraja fulani.
Marehemu Magufuli, kwa kiasi kikubwa aliharibu na wala hakuzingatia kanuni za uteuzi. Akazigeuza nafasi za wakurugenzi kuwa za kisiasa, na hivyo sehemu nyingi akawaweka makada badala ya kuwaweka wataalam.
Ombi letu ni kukuasa Mh. Rais, kurudi kwenye kanuni na sheria inayokutaka kumteua mtu kuwa mkurugenzi kwa kufuata vigezo vilivyowekwa kisheria kuliko kuangukia kwenye dimbwi la uchafu lililoachwa na marehemu, la kutofkufuata sheria na kanuni.
Kiongozi makini huonesha njia. Kiongozi ni lazima uoneshe mfano katika kuzingatia sheria na kanuni kabla ya kuwataka wanaokufuata kufanya hivyo.