Rais Samia zingatia Sheria kwenye teuzi za Wakurugenzi wa Halmashauri, Miji, Manispaa na Majiji

We ni nyumbu tu kwa akili yako unataka kusema miaka ya nyuma wale wakurugenzi hawakuwa makada ya CCM? Jua kabisa kama mkurugenzi kikatiba anateuliwa na Rais unaweza kusema hakuna siasa kwenye huo uteuzi? Au unajitoa ufahamu huku ukiwa na chuki kwa Marehemu. Kila kitu unalaamu mareheu hata ukishindwa mambo yako binafsi marehemu. Hivi umefanya nini cha maana baada ya marehemu kufariki?
 
Eti HASSAN NGOMA nae aliteuliwa kuwa DAS, aisee magufuli alikuwa anaiongoza nchi Kama kikundi Cha familia yake Chato
 
Aisee we Ni kichwa maji
 
Mtoa hoja na Kaka Paskal Mayala, Naunga mkono hoja. Sifa za Mtumishi kuwa MKURUGENZI WA HALMASHAURI NI LAZIMA AWE NA
1. ELIMU YA SHAHADA NA KUENDELEA
2. UZOEFU WA KAZI KATIKA NAFASI YA JUU (SENIOR POST) KWA MIAKA ISIYOPUNGUA 12. yaani toka aajiriwe km Afisa awe amefanya kazi kwa muda huo, hivyo lazima atakuwa na Cheo cha Afisa Mwandamizi Mkuu I au ii. Yaani ofisini tayari atakuwa Boss hivi wa Idara au kitengo. Au tayari ana heshima zake hapo. Ndio waliteuliwa kuwa Wakurugenzi na wengine MA-DAS pia. Pabakuwa hakuna lawama zozote.
Kitenfo kuteua kwa kigezo cha Chama tunaharibu mfumo kabisaaaaa. Ndio maana kwa CCM imejaa wanachama wenye malengo ya kunuifaika tu badala ya kukipenda Chama.
Mama taf aturejeshe kwenye utaratibu.
 
Maoni yako ni Mazuri. Lakini sio kila aliyeko kwenye siasa hawezi kuwa mkurugenzi. Wengine wengi tu wameingia kwenye siasa baada ya kuacha Kazi zao za kiserikali na bado wanafaa kurudishwa.
Yaani unamteua mkuu wa watumishi wa umma katika wilaya au manispaa ambaye cheki namba anaisikia tu redioni, acheni hizo...
 
T
Tuwe wa kweli aliyeanza kuvuruga Mambo Ni jpm...kikwete hakuteua wakurugenzi makada
 
T

Tuwe wa kweli aliyeanza kuvuruga Mambo Ni jpm...kikwete hakuteua wakurugenzi makada
Kikwete alianza utaratibu wa kuteua kupitia TAMISEMI. kukikuwa hd na Ma secondmaster, ambao hawana uzoefu kwa kazi hizo. Na washkaji pia walipata. Nilikuwemo tayari Council. Kabla yake, Mkapa hakuhusika na made. 2004 nilikuta matangazo ya nafasi za hixo ambapo watumishi waliomba, kusailiwa na baadae kuteuliwa. Yaani mnajua kabisa huyu at any time t atakuwa DED au DAS au Ahamishiwa RS kuwa RAS NA AS RAS
 
Maoni yako ni Mazuri. Lakini sio kila aliyeko kwenye siasa hawezi kuwa mkurugenzi. Wengine wengi tu wameingia kwenye siasa baada ya kuacha Kazi zao za kiserikali na bado wanafaa kurudishwa.
Ujinga
 
Sawa, lakini JPM ndo aliweka wazi kabisa, makada walioshindwa kwenye kura za maoni ndo wanapewa ukurugenzi.it was very bad kwa kweli
 
Wateuliwa wa Magufuli ni pure uchafu hamna wanachokifanya zaidi ya maslahi yao binafsi na kuendekeza maugomvi yasiyo na tija kisa mkurugenzi ni kada anatishia na kunyanyasa watumishi.UCHAFU MTUPU.
 
Ibara ya ngapi inasema Mkurugenzi anateuliwa na Rais?
 
Eti HASSAN NGOMA nae aliteuliwa kuwa DAS, aisee magufuli alikuwa anaiongoza nchi Kama kikundi Cha familia yake Chato
Huyu tayari kalamba teuzi ya uDC, haya makapu makubwa makubwa ya teuzi yanasheheni vichwa maji haswaaa kwa hizi teuzi za kubebana zisizozingatia sheria....
 
T

Tuwe wa kweli aliyeanza kuvuruga Mambo Ni jpm...kikwete hakuteua wakurugenzi makada
Hata RAS hawatakiwi kuwa wanasiasa. RAS ni nafasi ya kiutendaji kama ilivyo kwa katibu mkuu wa wizara. Ila naona mama kaendeleza mfumo wa JPM kiaina katuletea RAS makada. Tusubirie kuona teuzi za DED na DAS
 
Upo sahihi kabisa. Awamu ya Mkapa nafasi zilikuwa zinaombwa. Sijui kitu gani kilitokea awamu ya nne wakaanza kuteua, japo wateuliwa walitoka ndani ya utumisha wa uma. Waziri wa Tamisemi akawa maarufu sana, nakumbuka enzi za The Late Mama Kombani.
 
Baada ya Mwendazake kufa nina uhakika kuwa siwezi kutekwa na wasiojulikana. Halafu nina Uhuru wa kuongea na kumkosoa kiongozi yeyote bila kuogopa kushikwa na kunambikiziwa kesi.

Hayo tu yanayosha ambayo Rais SSH ametupa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…