John Haramba
JF-Expert Member
- Feb 4, 2022
- 365
- 1,374
Rais wa Senegal Macky Sall, ametangaza leo Jumatatu Februari 7, 2022 kuwa ni siku ya mapumziko maalum nchini kwake kwa ajili ya kusherehekea ubingwa wa Kombe la Mataifa ya Afrika #AFCON2021 waliochukua usiku wa kuamkia leo kwa kuifunga Misri kwa penati 4-2.
Sall, alikuwa njiani kwenda katika ziara nchini Comoros ambapo baadaye angeelekea, Misri na Ethiopia, lakini amesitisha ziara hiyo ili awapokee wachezaji hao wanaowasili nchini humo kutoka Cameroon.
Senegal waliongozwa na staa wa Liverpool, Sadio Mane ambaye alifunga penati ya ushindi katika ushindi wa penati 4-2 dhidi ya Misri iliyokuwa ikiongozwa na Mohamed Salah katika fainali, usiku wa kuamkia leo.