Rais sio mama aliyewanyonyesha watanzania. Anatakiwa asimamie nchi kwa mujibu wa katiba. Sio akikosea asikosolewe kisa ni mwananamke

Muuza Kangala

JF-Expert Member
Joined
Jul 21, 2021
Posts
1,242
Reaction score
4,813
Nimeona mahala kwenye mitandao ya kijamii rais wa JMT anasema watu wasipambanae kisa tu eti yeye ni mama. Hapa nafikiri anataka kupindisha mambo. Kwanza nafikiri hakuna anayependa kupambana na mkuu wa nchi bali watu huwa wanataka mambo yeende sawa kwa mujibu wa katiba ya JMT.

Lakini kama rais akiwa na jinsia ya kike alafu akaonekana kuna fyongo anafanya ndio watu wasihoji kisa tu mama?

Yaani kama kuna ukiukwaji wa haki za binadamu, ufisadi na uzembe unafanyika tusihoji na kukosoa kisa tu ni rais mwanamke ambaye kwetu ni maka mama?

Hii kauli haiko sawa. Raisa simamia katiba na ondoa viongozi wasiofaa bila upendeleo. Kukosolewa sio mapambano.

Hii kauli sio.
 
Mimi nilikataa kumuita Mama.

This is the infantilization of Tanzanians.
 
Weye naye kwa kulalamika haujambo.Acheni nchi itulie.Au tukuitie Ighondu na Mahita junior?
 
Kwa hiyo ilikuwa halali kupambana na baba ndiyo maana kafa kabla ya wakati wake? Daah
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…